Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,662
- 8,788
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema Mwigulu amesababisha matatizo makubwa kwenye SGR zaidi ya trilioni 4. Luhaga amesema Mwigulu hatakuwepo kwenye nafasi ya uwaziri labda kwa neema ya Mungu akidai hana sifa ya kukaa kwenye nafasi aliyonayo.
Mpina amedai Mwigulu amepiga ngonjera kwenye hotuba yake bila kuchukua hatua kwa watu waliokula pesa ya umma.
Mpina amesema Mwigulu anaingiza kodi ilhali kuna matrilioni hayajakusanywa na hasemi kwanini pesa husika hazijakusanywa. Mpina anadai Mwigulu anaenda kukopa pesa za semina na warsha kinyume cha sheria.
Mpina amesema kuongeza kodi kwenye mafuta na cement ni kupandisha mfumuko wa bei.
Pia, Soma=> Mwigulu amuwashia moto Mpina, ni kuhusu kufunga biashara. Adai Mpina anafurahia watu wakiumia