Mpenzi wa zamani wa rafiki yangu ananitaka kimapenzi, nifanyeje?

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,584
48,743
Naombeni ushauri,

Kusema kweli nilikuwa nawashangaa wadada marafiki wanaopokezana wapenzi kama mbio za kijiti ila leo yamenifika.Ninae shost wangu flani hivi yeye na mpenzi wake wameshindwana.

Alikuwa ananishtakia sana namshauri ila naona mwenyewe kafika mwisho akaona isiwe tabu akamuacha jamaa akaenda tena nje ya nchi kwa sasa anasema hatorudi tena ila mimi sijui mbeleni. Issue ilikuwa jamaa mlevi na michepuko ila yule best wangu alikuwa mtu mshari sana sana so kila siku kugombana sasahivi huyu bwana ananitaka sana.

Najua ni vibaya hata mi simtaki ila jamaa ni mzuri hb pesa zipo sana tu hata ikitokea nipo nae msema kweli mpenzi wa Mungu ni kuvuta mihela tu maana jamaa mtoaji sana sio bahili.Kitandani sio maana shost wangu aliniambia hakuna kitu dakika moja kule hoi hata alikuwaga na mchepuko wake.

Naombeni ushauri maana sina mpenzi wala sifikirii mambo ya wanaume ila maisha magumu na hili gunia la hela nisije lipiga teke.

Please msinitukane.
 
Have at it, for the money or whatever reason that may help you sleep at night...
U have what to give and so does he. The devil has always means to make things sour and when that time comes your way, just remember this-"it was just business!"
 
Sasa kama hautaki lipiga teke hlo gunia sasa unaomba ushauri wa nini?
 
Siku hizi naona mapenzi yameisha, nimejisikia vibaya sana kukutana na neno 'hela' kwenye story yako!
 
Ama kweli nimeamini baadhi ya wanawake hawawezi kujicontrol kwakua akili hawatembei nazo wenyewe huwa wanazikabidhi kwa watu Kisha anapotaka kufanya maamuzi hurudi kwa aliyemkabidhi akili zake amwambie cha kufanya. Watu wanataka ushauri, sawa!! Lakini c kwa jambo kama hili. Umeliona jibu halafu unatutaka tukusapoti kuhusu uzuri wa jamaa na mihela aliyonayo? Hivyo ni vipaumbele vyako wewe na c cc. Una dalili zote za Kuwa muuzaji na unataka na akili zetu zifanane na za kwako? Shost yako alikuambia kuhusu mambo ya kitandani na hayo mengine kamuulize yeye atakushauri vzr sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…