Anayetuhumiwa kumuua mwanariadha Rebecca Cheptegei naye aaga dunia akiwa hospitali

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
746
2,099
Ndiema.jpg

Dickson Ndiema, mpenzi wa zamani wa Rebecca Cheptegei, amefariki hospitalini.

Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha wa Uganda, marehemu Rebecca Cheptegei, ambaye alikuwa akituhumiwa kumuua kwa kumwagia petroli na kumchoma moto, amefariki kutokana na majeraha ya moto aliyoyapata wakati wa shambulio hilo.

Soma: Mwanariadha Uganda achomwa moto na mpenzi wake Mkenya, aungua kwa zaidi ya 75% ya mwili wake


Cheptegei, mwenye umri wa miaka 33, ambaye alishiriki kwenye mbio za marathon kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, alipata majeraha ya moto kwenye zaidi ya asilimia 75 ya mwili wake katika shambulio la Septemba 1, na alifariki siku nne baadaye.

Mpenzi wake wa zamani, Dickson Ndiema Marangach, alifariki saa 1:50 usiku siku ya Jumatatu, alisema Daniel Lang'at, msemaji wa Hospitali ya Rufaa ya Moi iliyoko Eldoret, magharibi mwa Kenya, ambako Cheptegei pia alitibiwa na kufariki.

"Alifariki kutokana na majeraha yake, moto aliopata," Lang'at aliambia vyombo vya habari..

Cheptegei, aliyemaliza nafasi ya 44 jijini Paris, ni mwanamichezo wa tatu wa kiwango cha juu kuuawa nchini Kenya tangu Oktoba 2021. Kifo chake kimeangazia tatizo la ukatili wa majumbani katika nchi za Afrika Mashariki, hasa ndani ya jamii ya wanariadha.

Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa wanariadha wa kike nchini Kenya wapo katika hatari kubwa ya kudhulumiwa na kufanyiwa ukatili na wanaume wanaovutiwa na fedha zao za zawadi, ambazo zinazidi vipato vya ndani.

Karibu asilimia 34 ya wasichana na wanawake wa Kenya wenye umri wa miaka 15-49 wamewahi kufanyiwa ukatili wa kimwili, kwa mujibu wa takwimu za serikali za mwaka 2022, ambapo wanawake walioolewa wako kwenye hatari zaidi. Utafiti wa mwaka 2022 uligundua kuwa asilimia 41 ya wanawake walioolewa wamepitia ukatili.

Pia, soma: Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyechomwa moto na mpenzi wake kutoka Kenya afariki dunia

========

The former partner of Ugandan athlete Rebecca Cheptegei, who is accused of killing her by dousing her in petrol and setting her on fire, has died from burns sustained during the attack, the Kenyan hospital where he was being treated said on Tuesday.

Cheptegei, 33, who competed in the marathon at the Paris Olympics, suffered burns to more than 75% of her body in the Sept. 1 attack and died four days later.Her former boyfriend, Dickson Ndiema Marangach, died at 7:50 p.m. (1650 GMT) on Monday, said Daniel Lang'at, a spokesperson at Moi Teaching and Referral Hospital in Eldoret in western Kenya, where Cheptegei was also treated and died.

"He died from his injuries, the burns he sustained," Lang'at told Reuters.

Cheptegei, who finished 44th in Paris, is the third elite sportswoman to be killed in Kenya since October 2021. Her death has put the spotlight on domestic violence in the East African country, particularly within its running community.

Rights groups say female athletes in Kenya are at a high risk of exploitation and violence at the hands of men drawn to their prize money, which far exceeds local incomes.

Nearly 34% of Kenyan girls and women aged 15-49 years have suffered physical violence, according to government data from 2022, with married women at particular risk. The 2022 survey found that 41% of married women had faced violence.

Reuters
 
Ukiua kwa upanga nawe utakufa kwa upanga! Jehanamu inamstahili akawe kuni za kuchomea wenye tabia kama zake
 
Dickson Ndiema aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei, aliyefariki baada ya kuchomwa moto na yeye, amefariki dunia kutokana na majeraha ya moto, kwa mujibu wa afisa wa hospitali nchini Kenya ambako alikuwa akitibiwa.
1725967284267.png
Ndiema amefariki akiwa ICU katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH) mjini Eldoret, ambako alikuwa amelazwa. Ndiema alipelekwa hospitalini baada ya kupata majeraha ya moto aliyoyasababisha alipomchoma moto Cheptegei.
1725967320187.png
Ndiema alimvamia mwanariadha huyo wa mbio ndefu alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kanisani zaidi ya wiki moja iliyopita, kisha akamwagia mafuta ya petroli na kumchoma moto, mbele ya watoto wake wawili.

Wawili hao walikuwa wakigombana kuhusu ardhi kaskazini-magharibi mwa Kenya, ambako Cheptegei alikuwa akiishi na kufanya mazoezi, kama walivyoeleza viongozi wa eneo hilo.
1725967369409.png
Cheptegei alipata majeraha ya moto kwa zaidi ya asilimia 80 ya mwili wake, huku Ndiema akipata zaidi ya asilimia 30 ya majeraha. Mwanariadha huyo alifariki katika hospitali hiyo hiyo, siku tatu baada ya tukio la kutisha lililotokea katika Kaunti ya Trans Nzoia.
 
Sasa kapata faida gani huyo mwehu..?? Unagombania kipande cha ardhi ambacho siku moja ubavu wako utakuja kukilala!!

Mali zote tunazomiliki wanadamu sio zetu, ni za warithi wetu ambao nao watakufa na mwisho ulimwengu ataurithi yule aliyeuumba.
 
Dem sura mbaya kauwawa na lijamaa nalo sura mbaya, kwa sura hiyo jamaa alikuwa anamuona dem kama malkia *****
 
Back
Top Bottom