"Mpenda sifa haachi kutapatapa"

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Siku zote mtu anayependa sifa atahangaika na watu kuliko mfumo ili watu hao waonekane wabaya na yeye aonekane mzuri.

Mpenda sifa hujiona yeye ni bora na mwenye haki ya kizalendo zaidi ya wengine. Yote hii kutafuta sifa za kipekee.

Mpenda sifa yuko radhi awatose wote abaki pekee yake akiogelea sifa.

Mpenda sifa huona wivu kwa wengine wenye nacho zaidi yake. Na atafanya kila namna kuwashusha chini zaidi yake ili abaki yeye juu.

Mpenda sifa hana jema analoliona kwa wengine. Yuko radhi akusaliti ili apate sifa bila kujali wema na fadhira alizopata toka kwa watu.

Mpenda sifa hujinasibu kwa nguvu na uwezo hata kama uwezo huo hana. Na mambo yanapomuendea kombo hutafuta mbaya miongoni mwa wanaomzunguka badala ya kubadili mbinu. Yeye sifa ni bora zaidi ya chochote.

Mpenda sifa anajulikana.
 
Umelenga kweli.

Mpenda sifa akiwa na madaraka anakuwa dikteta

Mpenda sifa hujiona ana akili kuliko watu wengine wote

Mpenda sifa anataka asemalo liwe. Hashauriki

Mpenda sifa siku zote huishia pabaya

Mpenda sifa huzungukwa na wanafiki wasioweza kuhoji chochote

Mpenda sifa hupenda kusifiwa tu. Kumkosoa ni kutafuta balaa kubwa

Hufika mahali akaona katumwa na Mungu kuja kuwaokoa watu wake
 
Hivi ungejisikiaje kama ungemaliza kuandika haya ukasikia kuwa Lowasa ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama haya yataifanya Chadema kwenda ikulu basi sawa......
 
Umekosea jukwaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…