Mpatie vyakula hivi kuepuka Mtoto kula mchanga na mjamzito kula udongo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,458
50,999
Kuna hii tabia ya wajawazito kula udongo na watoto kula mchanga huwa sipendi sana kuona wazazi wanawaachia watoto kula mchanga wengi wetu nadhani hatujui madhara yake. Kwanza kuna kupata maambukizi ya vimelea maana kwenye udongo kuna bacteria wengi, kama mtoto anaweza pia kukabwa au kupaliwa na mchanga, unaweza ukala sumu au utumbo ukajifunga ndani huko.

Kwanini ule vitu visivyo chakula, kama vile uchafu na vitu hatari. Nyie wanawake mnashindwaje kuacha kula udongo wa pemba. Wengine wanatafuna chaki, makamasi,sabuni, nywele, makaratasi wengine Mpaka vinyesi hii sasa si itakuwa ni kama ugonjwa wa akili..

Mara nyingi chanzo chake huwa ni ukosefu wa Madini ya zinc, vitamin b12, na chuma ambayo unatakiwa uyapate kwenye Lishe ya vyakula vifuatavyo samaki,samaki chaza, spinach, karanga, matikiti, matango, maziwa, mayai n.k..

images (16).jpeg
images (7).jpeg
images (14).jpeg

Mimba zangu zote sijawahi kula udongo au vitu vichachu......
Vitu vyangu pendwa nikiwa na mimba Kilimanjaro, nyama choma ya mbuzi samaki achemshwe na chumvi tu, mihogo , maini, maji niyawekee limau na kiugali cha muhogo. Nimemiss heka heka za mimba.
 
Kilimanjaro! Acha utani, usalama wa wapanda mlima huo ukoje! Au usalama wa wachaga nao ukoje.
 
Mimba zangu zote sijawahi kula udongo au vitu vichachu......
Vitu vyangu pendwa nikiwa na mimba Kilimanjaro, nyama choma ya mbuzi samaki achemshwe na chumvi tu, mihogo , maini, maji niyawekee limau na kiugali cha muhogo. Nimemiss heka heka za mimba
Bora wewe hata😆😆😆Mimi hupenda kula wali na maharage na kumung'unya unga wa ugali (Kama msukule😆😆😆)loh!
 
Back
Top Bottom