Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 308
- 1,352
Januari mwaka 2001 mapema kabisa kabla ya George Bush kuapishwa na kuwa rais wa Marekani, makamu wa rais, Bwana Dick Cheney alimtumia ujumbe waziri wa ulinzi, William S. Cohen ambaye aliwekwa hapo kupitia Chama cha Republic ambaye kwa wakati huo alikuwa akifanya kazi na Rais Bill Clinton aliyetoka Chama cha Democcratic.
“Tunataka kumpatia kwa ufupi sana rais mtarajiwa juu ya mambo fulani,” alisema Cheney.
Alisema hayo kwa kuwa alitaka kuona mazungumzo yaliyo serious yakifanyika juu ya Iraq ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kikwazo kikubwa. Kumbuka kwamba Saddam Hussein alikuwa anawavuruga vichwa.
“Rais ajaye hatakiwi kupewa kazi kubwa sana kwa mambo mengine bali anatakiwa kuliangalia sana suala la Iraq,” aliongezea.
Huyu Cheney alikuwa waziri wa ulinzi wakati wa Rais H.W. Bush (Baba yake George Bush) ambaye pia alihusika katika Vita vya Ghuba mwanzoni mwa miaka ya 90 na aliona kabisa kulikuwa na kazi ambayo haikumalizwa, ilikuwa ni lazima imalizwe na rais ambaye angeingia madarakani kipindi hicho.
Hii kitu nishawahi kuwaambia huko nyuma kwamba vita na Iraq ilikuwa ni lazima ipiganwe tena na Saddam atolewe madarakani.
Kwa nyongeza ni kwamba Iraq ilikuwa nchi pekee kipindi hicho kupigwa mabomu mengi na Marekani kuliko nchi yoyote ile.
Marekani ilipigana na Iraq kwa muda mrefu katika vita ya Ghuba kwa kipindi kirefu tangu baba yake Bush alipokuwa rais wa nchi hiyo. Umoja wa Mataifa haukuzungumza kitu, ulisapoti kile ambacho Marekani alikuwa akikifanya.
Miaka hiyo kwa kupitia nchini Kuwait, Marekani alikuwa akimshambulia Iraq, hakutaka kuona ndege yoyote ya nchi hiyo ikitumia anga lolote kwa ajili ya kupambana, yaani walitakiwa kukaa ardhini kupigana na mtu aliyekuwa akitumia ndege.
Kuwait alishirikiana na Marekani, nchi yake ilitumiwa kumpiga jirani yake. Hapa ni kwamba Waafrika na Waarabu, wote wanafiki, wote hatupendani, tupo radhi kumuona jirani yetu akishambuliwa na kuteketezwa kabisa.
Cheney na wenzake walitaka kwanza Bush afahamu masuala ya vita, ajue anakwenda kuwa rais wa Marekani lakini kulikuwa na lipi mbele ambalo alitakiwa kupambana nalo. Ilikuwa ni lazima kumpanga kwa kila kitu.
Ukiachana na hilo, pia katika muswada aliopelekewa Clinton mezani kwake, ilikuwa ni kusaini pendekezo la kuongeza pesa kwa ajili ya kwenda kupambana na Saddam Hussein.
Muswada huo ulisainiwa mwaka 1998 na ikapitishwa na bunge, kiasi cha dola milioni 97 kikapelekwa vitani kuhakikisha Saddam Hussein anang’oka na kuuawa mara moja.
Jumatano asubuhi, Januari 10, siku 10 kabla ya kuapishwa kwa George Bush, Cheney, Rumsfeld, Rice na Colin L. Powell walikwenda makao makuu ya kijeshi, Pentagon kukutana na Cohen.
Wakati huohuo Bush na timu yake walikwenda huko kuhakikisha kikao hicho cha siri kinafanyika kwa kukutana na viongozi wote wa kijeshi na kuzungumzia masuala hayo ya vita na Iraq.
Kutokana na kipindi kirefu cha kampeni, kuzunguka huku na kule, Bush hakuwa sawa kiafya ila alikuwa humo kwa kuwa tayari alishinda uchaguzi na kuwa rais, alisubiriwa kuapishwa na hatimaye kuwa rais wa nchi hiyo.
Humo ndani, majeneral wawili wa kijeshi wakaanza kutoa taarifa zao kuhusu Iraq kwamba....
Walizuia anga nzima ya nchi hiyo, hakukuwa na ndege yoyote ile kupaa lakini pia walihakikisha wanawalinda Wakurd kwa nguvu zote. Kwa mwaka uliopita, ndege za kijesi za Marekani na Uingereza zilikuwa zikizunguka kwenye anga la Iraq kwa siku 164 mfululizo kwa miaka ya nyuma
Karibia mwaka mzima ndege zao zilikuwa zikishambuliwa na Iraq kwa kutumia ulinzi wao madhubuti kwenye masuala ya anga lakini kwa kuwa walikuwa na nguvu, walikuwa wakirudisha mashambulizi kwa kiasi kikubwa.
Marubani walifanya kazi zao kwa kiasi kikubwa kuingia Iraq, zaidi ya mara 150,000 kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Na kwa mwaka uliopita tu, waliingia mara 10,000. Kumbuka taarifa hiyo ilikuwa inatolewa mwaka 2001.
Katika mashambulizi zaidi ya mia moja, marubani wa Marekani walipoteza kwa kupigwa vibaya. Pentagon walijaribu kupambana nao kwa nguvu kwa kutumia ndege kubwa za kijeshi.
Kwa kuunda ndege nyingi na zenye nguvu, zilitumika pesa nyingi, zaidi ya mamilioni ya dola. Ndege zao nyingi zikalipuliwa kwa kuwa inaonekana Saddam alikuwa na nyumba maalumu ya kuhifadhia silaha zilizokuwa na nguvu ambazo zilipambana na wanajeshi wa kwenye ndege zao.
Sasa hapa kukawa na swali, je, Bush angekubaliana nao katika suala zima la kupigana na Saddam na kumsambaratisha? Je, kwa sera ya nchi kwenye masuala ya ulinzi, hili liliruhisiwa ama walitakiwa kulifanya tit-for tat?
Huu mpango wa mzima wa kuivamia Iraq na kumuonda Saddam waliuita Desert Barger, yaani kipindi hiki wangepeleka ndege zao makusudi kwenye anga la Iraq, kama zingepigwa, basi hakukuwa na sababu ya wao kubaki kimya.
Na walijua tu lazima zitapigwa. Kwenye huu mpango, walijua kabisa Saddam alipenda kuchukua mateka marubani wa Marekani, sasa kipindi hiki walitaka kuonyesha walikuwa na nguvu ya namna gani.
Pia kukawa na mpango wa pili ambao waliuita Desert Thunder, huu ulikuwa ni mpango wa kumpiga Saddam kama tu angekwenda Kaskazini mwa Iraq na kuwapiga Wakurds.
Kulikuwa na mipango mingi iliyopangwa lakini yote hayo wala hayakuwa mageni kwa Chimney, Rumsfeld na Powell ambaye alitumia miaka 35 kuwa jeshini na aliwahi kuwa mwenyekiti wa Joint Chief of Staff kutoka 1989 mpaka 1993.
Rais ajaye, Bush alitakiwa kuuliza maswali kadhaa juu ya namna gani mambo yalitakiwa kufanyika lakini wala hakuuliza maswali, ndiyo kwanza akachukua pipi, akazifungua na kuanza kuzimung’unya.
Baadaye akamwangalia Cohen na kumuuliza “Unataka hizo pipi?” Cohen akasema hapana, Bush akazisogelea nyingine na kuzichukua. Baada ya karibu lisaa limoja na nusu, mwenyekiti wa Joint Chiefs, General Henry ‘Hugh’ Shelton akagundua Bush alikuwa bize kuziangalia pipi zake, akaamua kumpa.
Rumsfeld ambaye alikaa mwisho kabisa wa meza alitulia akiwasikiliza mtu waliyekuwa wakitoa brifling ya kikao hicho ingawa mara kwa mara aliwaambia waongeze sauti asikie vizuri.
“Tumeanza vyema,” alisema mmoja wa chiefs.
“Makamu wa rais amesinzia huku mkuu wa ulinzi akisema hasikii,” alisema Cohen ambaye alikuwa amebakiza siku 10 tu kuachana na cheo hicho na hatimaye kuja mtu mwingine kuchukua nafasi yake.
Aliamini kulikuwa na mengi ambayo mtu ambaye angechukua nafasi yake asingeyaona kwanza, asingekuta mengi yaliyopo na ilikuwa ni lazima kusaidiana na nchi nyingine la sivyo wangejikuta wakiwa peke yao kupambana na mtu mwenye nguvu kama Sadda Hussein.
Wangefanya nini kupambana naye angani? Alikuwa na uwezo mkubwa wa kuzipiga ndege zao, nini kifanyike? Alilifikiria hilo.
Cohen aliamini timu mpya ambayo ingeingia chini ya Bush ni lazima ingetafuta maridhiano na Saddam ambaye alihisi kutengwa na Waarabu wenzake.
Kama unakumbuka miaka mitatu tangu Bush achukue madaraka, alisimama na kusema hakuwa na furaha na sera za nchi ya Marekani. Hazikuwa imara za kumfanya Saddam kubadilika.
Na kwa sababu hiyo, atahakikisha anakuwa kifua mbele kuhakikisha mwanaume huyo anaondoka haraka madarakani ama kumpoteza kabisa.
Okay! Turudi kipindi hicho cha kikao.
Itaendelea