Paul lubinza kulwa
New Member
- May 30, 2024
- 1
- 1
Moja ya changamoto kubwa nchi Tanzania ni mmomnyoko wa maadili kwa watanzania hasa vijana wengi wa kizazi hiki unaotokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano(UTANDAWAZI).
Tukiwa kama Taifa linaloendana na mabadiliko haya ya dunia jamii ya Tanzania haina budi kuandaa mikakati itakayolenga kupambana na athari za utandawazi katika kuharibu mila na desturi za Taifa letu ambazo ndio nguzo kuu ya kujenga jamii yenye maadili mema.
Zifuatazo ni mbinu muhimu katika kuhakikisha tunalinda na kuhifadhi mila na desturi bora za Taifa letu ili kuepuka kuwa na jamii isiyokuwa na maadili mema
Kuandaa mfumo wa elimu unaozingatia kuwaelimisha vijana juu ya tamaduni za Kitanzania na Afrika kwa ujumla;
Serikali ya Tanzania inapaswa kuandaa mfumo bora wa elimu ambao utatoa mwongozo wa kuwafundisha wanafunzi Tamaduni za kitanzania na kiafrika ili kufanya kuwa na mwendelezo bora wa jamii inayozingatia maadili mema na utu ikiwa ndio kielelezo kikuu cha mwafrika, hii ifanywe kwa namna ya kuandaa masomo maalumu yenye historia za watu mashuhuri wa kitanzania waliozingatia tamaduni kama vile viongozi wa kisiasa na viongozi wa kitamaduni pamoja na wasanii walioelimisha jamii kwa kuzingatia maadili mema kama vile Mrisho mpoto na Hamisi Mwinjuma maarafu kama Mwana FA, ambaye ni kati ya wasanii waliofanya sanaa zao kwa kutumia lugha yenye staha na kupeleka ujumbe mahususi kwa jamii bila hasa katika kuwatia moyo watanzania katika kupambana na mambo kadha wa kadha ili kujikwamua kiuchumi na kifikra
Kuandaa maonyesho yenye kubeba jumbe za kitamaduni zaidi;
Huu utakuwa muendelezo bora zaidi katika kudumisha tamaduni za kitanzania,serikali inapaswa kuandaa maonyesho ya kila mwaka katika kila kona ya nchi(wilaya na mikoa) yatakayolenga kutoa ujumbe wenye maadili mema kwa jamii kama vile ngoma za kiutamaduni na michezo mbalimbali ambayo inabeba historia ya jamii husika ili kukuza na kutoa fursa za vijana kujifunza maadili yetu ya kihistoria. Hii inapaswa kuandaliwa na maafisa utamaduni wa kila wilaya au mkoa ili kutoa fursa kwa washiriki wa eneo husika na tangu hapo watu watapata elimu na kujifunza zaidi katika maonyesho hayo mfano mzuri ni maonyesho yanayofanyika katika mkoa wa shinyanga wilayani kishapu katika maadhimisho ya sikukuu za nanenane kila mwaka.
Kutengeneza kamati za maadili kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Taifa; Kamati hizi ziwe na lengo moja tu la kudumisha mila desturi za taifa letu na kuhakikisha kizazi kipya kinaishi kwa kufuata taratibu zote za kitanzania, kamati hizi ziwe majukumu ya kusaidia katika masuala ya kisanaa hasa katika sanaa za kitamaduni kwani ni moja kati ya sehemu zilizosahaulika na baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kwani jamii kama ya kisukuma inaoa wasanii wengi sana wanajihusisha na utungaji wa nyimbo na utumbuizaji lakini wengi wao wanatumia lugha isiyo na maadili na hawachukuliwi hatua yoyote hivyo kuchangia kuwa na jamii isiyo na maadili kuanzia katika ngazi ya jamii ndogo hatimaye Taifa lote.
Kuwe na miongozo bora juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii(social medias); Miongozo hii iwe yenye kuzingatia umri wa mtumiaji ipasavyo kama vile kuweka namba ya NIDA au kitambulisho cha taifa kila unapotaka kujisajiri katika kila mtandao wa kijamii ili kuweza kutoa taarifa sahihi za umri na makazi na mtumiaji anapokiuka matumizi sahihi ya mitandao achukuliwe hatua sitahiki.
Kuundwa kwa Wizara Mpya itakayojikita na masuala ya kitamaduni;
Kama ilivyo kwa wizara nyingine ambazo zimeundwa kwa lengo la kujipambanua katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii, pia kuna uhitaji mkubwa wa kuanzisha wizara ya utamaduni peke yake ili kuepusha muingiliano wa majukum katika kufautilia masula ya mila na desturi kama ilivyo sasa kwani wizara inajikita kwenye michezo ya mpira wa miguu huku ikiwa imesahau upande wa pili wa utamaduni wa mtanzania ukiangamia na kupelekea kuwa na taifa lisilo na uelekeo
Kutilia mkazo somo la Historia ya Taifa kuanzia shule za msingi hadi elimu za juu; Hii ni kwa sababu taifa bila historia ni sawa na kukosa uelekeo kwani unapotaka kuijua kesho yako lazima uijue jana yako yako Taifa letu limekosa somo ambalo litatoa mwongozo kwa watoto juu ya wapi tulikotoka na zaidi yake tunajikita kufundisha historia ya wakoloni pamoja na mabepari kitu ambacho hakijengi msingi imara juu ya kuheshimu mila na tamaduni zetu mfano mzuri kuanzia kidato cha kwnza hadi cha sita ni maada chache sana zinazozungumzia historia ya mwafrika au mtanzania ikiwa maada nyingi zimejikita kueleza habari za ukoloni na kuibua madhaifu ya jamii za kiafrika huku zikisifu mataifa yaliyotutawala