Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,913
- 35,585
Mpaka muda huu naandika, ukitoa Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkuu wa mkoa wa Dar ndiyo wanasiasa wa juu pekee ambao wameongea chochote kuhusu kuungua kwa soko la Karume Ilala.
Pamoja na kwamba Dar ina wabunge bao ndiyo wa karibu mno na wafanyabiashara hao, lakini wameamua kuwapotezea. Rais wa Nchi ambaye ndiye mfariji mkuu kwa mujibu wa taratibu za kiserikali, naye amekuwa kimya mno kwenye hili.
Waziri Mkuu ambaye ana mfuko wa Majanga na Dharura naye hakuthubutu kusema lolote tofauti na lilivyoungua soko kuu la Kariakoo. Hii hali inasababisha dukuduku kubwa na kutoondoa hisia za wanajamii kuhusu yaliyo nyuma ya pazia kuhusu kuungua kqa soko lile.
Pia hata haraka iliyotumika kutuma watu kwenye media kutengeneza taswira kuhusu chanzo cha moto, kwa wenye akili wanapata majibu ya nukta zilizoanza kujijenga tangu moto unaanza na kutekeza kila kitu ilihali ni umbali usiozidi kilometa 3 kutoka kituo kikubwa cha zimamoto.
MPANGO WA DHARURA
Pamoja na hayo yote, bado ingalipo nafasi kwa serikali kujenga taswira ya kujali na kuaminika.kwa wananvhi wake
Kwanza ikumbukwe kuwamba, soko la Karume linachangia saba kwenye mwenendo wa mzunguko wa fedha na kupunguza jobless na umasikini nchini. Pia linatumika kama "feeder" kwa wafanyabiashara wa mikoani na nchi jirani kwani wanakuja kununua mizigo ya jumla pale.
Wasafirishaji mizigo wameathirika sana kutokana na wateja kukatika ghafla kutokana na kuungua soko hilo.
Mabenki yameingia loss kubwa kwa sababu, wafanyabiashara wengi walichukua mikopo kukuza mitaji yao pale sokoni. Uwezekano wa fanilia nyingi kuathirika kupitia dhamana zao benki upo wazi sana
Familia za waathirika zinapitia wakati mgumu kwani tegemeo lao limegeuka jivu kwa saa chache.
Athari zake
1. Uhalifu kuongezeka (jobless)
2. Kuongezeka kwa maradhi ya stress
3. Uchumi wa nchi kuathirika
4. Tishio la ugaidi au vurugu
Nini kifanyike
Ninaishauri serikali kuangalia uwezekano wa kutumia fedha ya dharura kupitia ofisi ya Waziri mkuu kufanya yafuatayo
1.
Kupitia orodha ya wachuuzi hapo sokoni, kutoa mikopo isiyo na riba kwa waathirika wote soko la Karume Ilala
2.
Kupeleka bungeni mabadiliko ya sheria ya fedha 2021/2022 kwa kuwaongeza waathirika wa soko la Karume kwenye wafaidika wa mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam
3.
Kuufunga uwanja wa mpira wa Karume kwa muda maalumu na kuwapanga wafanyabiashara mule ndani wakati serikali inarekebisha miundombinu ya soko lililoungua.
Ninaleta haya maaoni yangu hapa kwa sababu najua viongozi wakuu wanapitia hoja zetu hapa jukwaani na hata mawazo ya wanaJF wenzangu yanaweza kuiboresha ama kuipinga hii hoja kwa haki kabisa.
Msanii
Mfanyabiashara soko la Karume Ilala