Mlundilwa Jr
JF-Expert Member
- Dec 11, 2019
- 3,104
- 4,706
Wakuu habari,
Mpangaji mwenzangu amehama kisa shughuli zangu zinazoniingizia kipato zinamkera.
Nikawaida kukuta kwenye hizi nyumba za kupanga kukuta watu wakifanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato ili maisha yaendelee na kuweza kulipa kodi.
kuna wengine ktk hizi nyumba za kupanga huwa wanakaanga samaki, wengine wanachoma vitumbua, wengine chapati wengine huuza ice cream ivyo yaani.
Sasa mimi kazi ninayofanya ninacheza na moto kwamaana hiyo kivyovyote moshi lazima uwepo sasa huu moshi ndiyo umekua tatizo kwa mpangaji mwenzangu na kupelekea kuhama nyumba.
Alipeleka malalamiko kwa mwenye nyumba ili nipewe notes nihame nakweli mama mwenye nyumba kwakua haishi pale aliamuru kodi ikiisha basi nifungashe virago niondoke.
Ila kuna kibanda najenga na sijakimaliza hivyo nikamuomba anivumilie hadi mwakani ili nikiondoka basi niende kwangu ingawa aligoma kupokea ombi langu, mimi nilichofanya nikamlipa kodi nyingine kwa kufosi ingawa alitaka kunirudishia ila walikaa kama familia wakakubaliana nikae hadi apo muda utakapo fika nihame.
Sasa mpangaji mwenzangu alivyosikia nimeongeza kodi, aisee leo naamka nakuta chumba kipo wazi hata kuniaga hajaniaga. Huyu kijana yeye ni mwalimu na anamke ukimuona ni Mpole ila ndani ni simba.
Hiyo ndiyo hali halisi wakuu, tujitahidi kupambana ili tuwe na kwetu lasivyo unaweza kuta unatolewa vyombo nje mchana kweupe kisa fulani ktk hiyo nyumba unamuharibia mazingira.