JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,666
- 6,427
Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kiloleni ambapo Wananchi wa maeneo hayo walitii wito wa kutoka katika Hifadhi ya Msitu wa Kijiji na sasa wanaomba kuongezewa eneo la kufanya shughuli za kilimo ili kuendelea kujikimu kimaisha.
Damas Ngassa ni Afisa Ardhi wa Halimashauri ya Nsimbo amesema mipaka ya kijiji bado ni ileile na inapaswa kuheshimiwa huku Adam Chalamila ambaye ni diwani wa Kata ya Sitalike amesisitiza kuwepo kwa mpaka wa msitu wa kijiji hicho na kuiomba Serikali kupeleka huduma za kijamii katika kijiji chicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf mbali na kufurahishwa na utii wa wananchi hao wa kutoka katika msitu wa kijiji hicho lakini amewataka wananchi wa kijiji cha Kiloleni kuheshimu mipaka iliyowekwa na serikali pamoja na utunzaji wa misitu.
Mbali na hayo ametoa agizo la kuhakikisha vibanda vyote vilivyoko katika hifadhi ya msitu wa kijiji kuondolewa haraka.
Katika hali hiyo Jamila ametangaza oparesheni maalumu ya kuhakikisha kila mwananchi kuwa mlinzi wa utunzaji rasimali ya misitu ikiwemo kupanda miti.