Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,490
- 4,774
tarehe 19 ya mwezi augasti mnamo mwaka 1969 Nathaniel Dwayne Hale alizaliwa ktk viunga vya Mississippi nchini Marekani na baadae makuzi yake yote katika uhai wake aliishi Long Beach California.
na muda ulipojiri basi ikawa kama bahati ndipo alipokutana na wasanii kama Snoop Dogg, Kurupt Dogg, Daz Dillinger na mtu ambae walishirikiana kwa kipindi kireefu sana katika harakati zao za Muziki yaani Warren G.
mpaka kufikia hapo jina la Nathaniel likawa limezikwa na kuzaliwa jina alilokuja kudumu nalo mpaka siku aliposhindwa kufumbua macho yake na kutuacha washkaji zake na wapenzi wa kazi zake tukiwa kwenye majonzi makubwa mno.
hapa namzungumzia mfalme wa Chorus katika miondoko ya G-funk, hip hop,
West Coast hip hop,
Gangsta rap,
Hiphop, soul na R&B.
namzungumzia
Rapper, Singer na Actor aliedumu kwenye game tangu mwaka 1992 mpaka mwaka 2011 akitamba na
lebo kama DeathRow, Elektra,
Doggystyle, Atlantic na Aftermath...
hapa namzungumzia mtu alieshirikiana kwa karibu na wasanii kama 2Pac, Dr. Dre,
Eminem,
Game, Tha Dogg Pound,
Xzibit, Obie Trice,
Warren G,
Westside Connection,
50 Cent
Snoop Dogg, Ice Cube, Ludacris,
MC Ren, WC na wengine kadha wa kadha, hapa namzungumzia Nate Dogg mzaliwa wa Mississippi aliehamia Long Beach, California akiwa na miaka 14 tu baada ya wazazi wake kukubali kuvunja ndoa yao.
huko Long Beach Nate alikutana na Warren G, RBX, Daz Dillinger na binamu yake yani Butch Cassidy sambamba na
Snoop Dogg. alianza kuimba akiwa bado mtoto katika kanisa la New Hope Baptist Church huko Long Beach ambako babaye yani Daniel Lee Hale alikuwa mchungaji na Mama yake Ruth Holmes alikuwa muimbisha kwaya Kanisaji hapo.
katika harakati za kutafuta maisha huku
akiwa na miaka 17 Nate Dogg aliachana na masomo yake ya elimu ya juu na kujiunga na jeshi la wana Maji nchini humo.
lakini mambo hayakumuendea vizuri na ilipofika mwaka 1990, Nate Dogg, Snoop Dogg ,
Daz Dillinger na Warren G, waliunda muungano uliotambulika kama 213, kisha wakarekodi demo yao ya kwanza ktk studio ya V.I.P huko Long Beach. Demo hio hatimae ikatambulishwa kwa mara ya kwanza na kaka yao yani Dr. Dre katika house party na kufanikiwa kubamba sana usiku huo.
miaka mitatu baadae jina la Nate Dogg lilikuwa ni jina kati ya majina na hatimae mwaka 1993 alisaini mkataba na studio ya Deathrow. mwaka uliofuata akiwa sambamba na rafiki yake wa karibu Warren G walishirikiana na kutoa ngoma iliojulikana kama regulate ambayo ilitumika kama Soundtrack ktk Movie ya above the rim.
mpaka kufikia hapo vilinge vya muziki nchini humo na Dunia vilikiri mbele ya hadhira kuwa Nate Dogg ana Golden Voice Vocal "GVV" na tangu hapo Nate akashirikiana na wasanii wengi wakubwa kama 2Pac 's "All About U", Dr. Dre 's " The Next Episode ," Westside Connection 's " Gangsta Nation," Mos Def 's "Oh No,"
Fabolous ' " Can't Deny It ," Ludacris' " Area Codes ," 50 Cent 's " 21 Questions," Kurupt's "Behind The Walls", Mark Ronson's "Ooh Wee,"
Houston 's "I Like That ," Eminem's " 'Till I Collapse", "Never Enough na Shake That ", pia Mobb Deep's alishirikiana nao katika ngoma iliojulikana kama Have a Party."
si hao tu Nate Dogg ameshirikiana na wasanii wengi wengine kama Xzibit, Eve, Shaquel Oneil, Jermain Dupri, Memphis Bleek, Obie Trice, Bishop Lamonte, Brian Mcnight, C-Murder, Black Robb, Dj Quick, Joe Burden, the D.O.C, knock turn,al, Lil Jon, Kokane, Lil flip, Loyd Bainks, Mariah Carey, Nelly, Outlawz, Ras Kass, Proof na B.I.G
orodha hio haija ambatanisha wasanii wawili ambao ni Warren G na Snoop Dogg. inaaminika kuwa Snoop Dogg na Warren ambae ni binamu wa Dr Dre walikuwa wakitumia nafsi 3 tofauti na roho moja ambayo kwa sasa ni half Dead. watatu hawa walielewana saana kiasi kwamba walishiriki kupishana katika verse na chorus nyingi za nyimbo zao. Snoop na Warren wamebaki wapweke sana, na ni kama tu kusema Snoop amebaki peke yake kwenye tasnia ya Muziki.
MWANZO WA MWISHO WA NATE DOGG.
mwezi December 19, 2007, Nate Dogg akiwa mzima na mwenye afya tele alishambuliwa na maradhi ya stroke maarufu kama kupooza. lakini kwa mujibu wa wana familia yake, Mfalme huyu wa Chorus aliruhusiwa kutoka Hospitali December 26 na kushauriwa kushiriki mazoezi ya tiba ambayo yangemuwezesha kurudi katika hali yake ya kawaida.
January 18, 2008, ilitangazwa rasmi katika vituo vya redio na televisheni mbalimbali Duniani pamoja na mitandao ya kijamii kuwa, Strock ya Nate Dogg ilimshambulia upande wa kushoto yaani upande uliopo Moyo. Madaktari waliamini kuwa Nate atarudi ktk hali yake ya kawaida na kuongeza kuwa sauti yake haikuathirika na ugonjwa huo.
lakini kwa bahati mbaya September 2008, Nate alishambuliwa tena na maradhi hayo.
picha ya mwisho ilimuonesha Nate Dogg akiwa kalala kitandani huku akiwa mwenye sura ya upole zaidi ya ule aliokuwa nao.
hata ilipojiri usiku wa Jumanne ya mwezi Machi tarehe kama ya leo yaani 15 mwaka 2011 huko Long Beach California Nate Dogg akiwa na umri wa miaka 41 alifumba macho na kukata roho.
katika ukurasa wangu wa Whatsapp nilipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa kutoka kwa nguli mwenzangu wa Hiphop akinijuza kuwa "NATE DOGG HAS GONE".
i was somewhere unknown smoking my stick na nilishindwa kuendelea. watu wa karibu niliokuwa nao pia walipigwa na butwaa baada ya kuona mshtuko nilioupata.
kwa masikitiko makubwa ya kupotelewa na kipenzi chetu nilianza kurudia kila ngoma aliosimama mwenyewe ama alioshirikishwa, na nilipofika ktk Chorus ya LayLow ilibidi niiweke simu pembeni kwanza, lakini machozi yalinimwagika baada ya kukumbuka Nate alipoingia kushiriki wimbo wa Next Episode wa Dr Dre katika Concert ya Up in Smoke mwaka 2001.
wakati nikiendelea kutafakari nikapokea twita ya Snoop... katika ukarasa wake wa Tweeter Snoop aliandika kwa uchungu maneno haya " “We lost a true legend n hip hop n rnb,”. “One of my best friends n a brother to me since 1986 when I was a sophomore at poly high where we met. I love u buddy luv.
U will always b wit me 4ever n a day u put the g n g funk u put the 1 n 213 n u put yo stamp on evrybdy u ever didit wit …
I miss u cuzz I am so sad but so happy I got to grow up wit u and I will c u again n heaven cuz u know d slogan All doggs go to heaven yo homie n baby brotha bigg snoopdogg!!”...
alimaliza Snoop Dogg
wakati Big Snoop Dogg akitangulia, aliefuata alikuwa Dazz ambae kwa majonzi aliandika
“R.I.P. TO MY HOMEBOY NATE DOGG DPGC DOGG POUND GANGSTA 4 LIFE,” Daz tweeted.
kama hio haitoshi Ludacris huku akikumbuka balaa alilolifanya Nate Dogg ktk Area Code ilibidi aandike “There is a certain void in hip hop’s heart that can never be filled. Glad we got to make history together. RT @SnoopDogg: RIP NATE DOGG,” Ludacris tweeted.
wakati alcoholic president yeye nae hakubaki nyuma na akaandika “I lost a friend, been here before.
Tears, Memories, One day someone will lose ’US’ as well.
LIVING until that day comes is our only option. R.I.P. Nate Dogg. Why does it take Death to remind us about the importance of life ??? Cherish every moment cuz tomorrow he mite call your #.” akamalizia kwa uchungu Xzibit
siku ya mazishi ilipofika maelfu wa wanafamilia na marafiki na wapenzi wa kazi za Nate walijitokeza kwa mara ya mwisho ili kutoa heshima zao kwa rap legend Nate Dogg , ambae umauti ulimpata huku ukiambatana na maumivu makali sana.
ndani ya ukumbi wa the Long Beach Cruise Terminal, taa ziliwashwa wakati jeneza lililombeba mpendwa wetu likiingizwa ukumbini huku likiwa limefunikwa kwa maua meupe na mekundu.
TV kubwa mbili zilizokuwa kila upande mbele ya ukumbi zilionesha picha sita tofauti za hayati tangu alipokuwa mdogo.
aliepata nafasi ya kuongea kwanza ukumbini hapo alikuwa Warren G ambae alisimama huku akiwa kaliinamia jeneza na kusema
“It hurts me so much to see this, we been through a whole lot and that was my dog.
He stayed down with me from the bottom to the top. I didn’t ever think I would have to sit at a funeral for one of my dogs.
All I can say is that was my friend, me him and Snoop was 213 from the balls to the walls. The music industry lost an incredible artist.”
aliefuata alikuwa ni snoop ambae nae akasema " “We didn’t know each other, but the music connected us. We built a brotherhood, a friendship.”
snoop, Warren G na Nate Dogg walikutana shule huku wakiwa vijana wadogo tu na walianzisha kundi la 213 na hakika walikuwa ni marafiki wakubwa sana.
Na muda wa maziko ulipojiri, mwili wa Nate Dogg ulisindikizwa na watu elfu moja tu ambao ndio walipata tiketi ya kuingia katika makaburi ya the Queen Mary Dome yaliopo huko Long Beach.
mapema taarifa iliorushwa ktk vyombo vya habari na halmashauri ya jiji la Long Beach zilitanabaisha kuwa tiketi kwa ajili ya kuingia kwenye makaburi hayo zitaanza kutolewa tarehe 25, Ijumaa ya mwezi Machi na mazishi yatafanyika Jumamosi ya Tarehe 26 ya mwenzi Machi na kumalizia kuwa yeyote asie na tiketi basi asifike ukumbini wala Makaburini.
baada ya Maziko msemaji wa Familia alisimama na kutoa shukrani zake za dhati kwa Dr Dre,snoop Dogg, Warren G, Xzibit na Eminen kwa kutoa mchango mkubwa sana katika kuokoa maisha ya Nate.
msemaji huyo alikwenda mbali zaidi na kurudia shukrani alizotuma Nate Dogg masaa machache kabla hajakata roho pale alipotuma salamu za upendo na shukran ziwafikie ndugu zake hao ktk Game ambao walimhudumia mshkaji wao huyo tangu mwanzo wa maradhi mpaka umauti.
wakati hayo yakitokea hakukuwa na salam za pole wala kujitokeza kwa mmiliki wa zamani wa Studio mfu ya Deathrow yaani Marion Suge Night.
Suge walifahamiana na Nate Dogg kwa muda mrefu sana na pia walifanya kazi pamoja.
R.I.P Nate Dogg
we will forever loving you.