Moshi: Mwanafunzi adaiwa kumuua mwenzake wakibishana umri

Analog

JF-Expert Member
Apr 4, 2024
278
530
Moshi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili (miaka 17) kwa tuhuma za kumuua rafiki yake, John Lema (18) chanzo kikielezwa kuwa, mabishano ya umri.

Mwanafunzi huyo mkazi wa Mtaa wa Kalimani, Wilaya ya Moshi inadaiwa yeye na Lema walikuwa marafiki na siku ya tukio walikaa kijiweni wakivuta sigara, wakaanza kubishana kuhusu umri kwamba nani mkubwa kati yao.

Inadaiwa kuwa, Lema alidai yeye ndiye mkubwa, jambo ambalo halikumfurahisha mwenzake aliyekuwa akidai ndiye mkubwa.

Inadaiwa baada ya mwanafunzi huyo kuona Lema anang’ang’ania ukubwa, aliamua kumshambulia kwa kumkata shingoni na mkononi kwa panga na kusababisha kifo chake.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Septemba 12, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea Jumatatu Septemba 9, mwaka huu, saa nne usiku, katika Mtaa wa Kalimani, eneo la Dampo, Kata ya Kaloleni, Wilaya ya Moshi.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni mabishano ya nani mkubwa kati ya marehemu na mtuhumiwa.

“Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi kwa uchunguzi wa kidaktari,” amesema kamanda huyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kalimani, Ndama Masule amedai kuwa, vijana hao walikuwa wamekaa kijiweni wakivuta sigara, ndipo mabishano ya umri yalipoanzia.

"Waliendelea na mabishano kwa muda mrefu; marehemu (Lema) akamwambia mtuhumiwa mimi ni kaka yako nisalimie, marehemu akasema hawezi kumsalimia shikamoo kwa sababu wangeenda wote sekondari wangekuwa darasa moja," amesema mwenyekiti huyo.

“Marehemu alimwambia mtuhumiwa, angekuwa anasoma kama yeye wangekuwa wote kidato kimoja, hiyo kauli ilimuudhi mwenzake akamshambulia kwa panga.”

Hata hivyo, amewasihi wazazi kukaa na kuzungumza na watoto wao wajue wanakabiliwa na changamoto gani ili wazitatue (hakufafanua zaidi).

Baba wa marehemu, Francis Lema amesema watoto hao walikuwa wanataniana, utani uliozua mauti kwa mmoja.

“Ulikuwa kama utani ambao uligeuka kuwa mabishano makali mpaka wakapigana mwilini, mtuhumiwa (anamtaja jina) alipoona anazidiwa nguvu, akakimbilia kuchukua panga na kumkata mwenzake shingoni na kiganja cha mkono, mwanangu amekufa, sina la kusema,” amesimulia baba huyo huku akibubujikwa machozi.

Hata hivyo, amesema maziko ya mwanawe yatafanyika kesho Ijumaa, Septemba 13, 2024, baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna watu sijui wao wanatembea na mapanga kila wanapo enda, kwamba wakiona nyasi nzuri wanakata na kupeleka nyumbani sasa hapo kwenye kijue cha cha bagi panga ni la kazi gani.
Vijana form 2&3, wamekaa usiku kijiweni, wanavuta "sigara" na panga mkononi..... 🤔

Nawaza kama kaweza kumjeruhi na kumuua rafiki yake, raia angejichanganya hapo mbele yake.
 
Moshi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili (miaka 17) kwa tuhuma za kumuua rafiki yake, John Lema (18) chanzo kikielezwa kuwa, mabishano ya umri.

Mwanafunzi huyo mkazi wa Mtaa wa Kalimani, Wilaya ya Moshi inadaiwa yeye na Lema walikuwa marafiki na siku ya tukio walikaa kijiweni wakivuta sigara, wakaanza kubishana kuhusu umri kwamba nani mkubwa kati yao.

Inadaiwa kuwa, Lema alidai yeye ndiye mkubwa, jambo ambalo halikumfurahisha mwenzake aliyekuwa akidai ndiye mkubwa.

Inadaiwa baada ya mwanafunzi huyo kuona Lema anang’ang’ania ukubwa, aliamua kumshambulia kwa kumkata shingoni na mkononi kwa panga na kusababisha kifo chake.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Septemba 12, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea Jumatatu Septemba 9, mwaka huu, saa nne usiku, katika Mtaa wa Kalimani, eneo la Dampo, Kata ya Kaloleni, Wilaya ya Moshi.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni mabishano ya nani mkubwa kati ya marehemu na mtuhumiwa.

“Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi kwa uchunguzi wa kidaktari,” amesema kamanda huyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kalimani, Ndama Masule amedai kuwa, vijana hao walikuwa wamekaa kijiweni wakivuta sigara, ndipo mabishano ya umri yalipoanzia.

"Waliendelea na mabishano kwa muda mrefu; marehemu (Lema) akamwambia mtuhumiwa mimi ni kaka yako nisalimie, marehemu akasema hawezi kumsalimia shikamoo kwa sababu wangeenda wote sekondari wangekuwa darasa moja," amesema mwenyekiti huyo.

“Marehemu alimwambia mtuhumiwa, angekuwa anasoma kama yeye wangekuwa wote kidato kimoja, hiyo kauli ilimuudhi mwenzake akamshambulia kwa panga.”

Hata hivyo, amewasihi wazazi kukaa na kuzungumza na watoto wao wajue wanakabiliwa na changamoto gani ili wazitatue (hakufafanua zaidi).

Baba wa marehemu, Francis Lema amesema watoto hao walikuwa wanataniana, utani uliozua mauti kwa mmoja.

“Ulikuwa kama utani ambao uligeuka kuwa mabishano makali mpaka wakapigana mwilini, mtuhumiwa (anamtaja jina) alipoona anazidiwa nguvu, akakimbilia kuchukua panga na kumkata mwenzake shingoni na kiganja cha mkono, mwanangu amekufa, sina la kusema,” amesimulia baba huyo huku akibubujikwa machozi.

Hata hivyo, amesema maziko ya mwanawe yatafanyika kesho Ijumaa, Septemba 13, 2024, baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
Hii ilikua bange sio sigara.
 
d9c324ceb36638002c7ae74f1e816670.jpg
 
Back
Top Bottom