Moshi: Amuua mama yake wakigombea mali za marehemu baba yake

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,772
18,417
Huko moshi jamaa wa miaka 54 amemuua mama yake wa miaka 74 kwa sababu ya ugonvi wa mali alizoacha baba ama mume wa marehemu ambae ndio baba wa mtuhumiwa.

Marehemu aliacha mashamba, hayo ndio yameleta mgogoro hadi jamaa akaamua kumuua mama yake.

Matukio ya hovyo ya watu kuua wazazi wao kisa mali yanashamiri sana Kilimanjaro.
---

Adela Mushi (74), mkazi wa Okaseni, kata ya Uru kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, anayedai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.

Inadaiwa kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 54, alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi.

Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaidi.

“Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, maeneo ya Uru Okaseni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Adela Dominick Mushi, aliuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic,” amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa , lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.

Mwananchi
 
Maisha magumu wazazi acheni ujinga wapeni watoto wenu mali wakasake life
Ajira hakuna
 
Nawaambien vijana wa humu, wanaojiita watoto na wana miaka 28-30 like hawajui kwamba kufumba na kufumbua 50 hii hapa kwenye kona na wamejaa mazima na mali yoyote ya maana hawana,mwisho wanaishia kuua ili kugombea mali.

Kijana usipokua makini, wewe ndio huyu huyu bwana baada ya muda sio mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…