Morogoro: Warsha ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Jukwaa la Wahariri (TEF) kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,770
121,827
Wanabodi

Niko hapa Morena Hotel Morogoro kuwaletea live, warsha ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Jukwaa la Wahariri (TEF) kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi.
TEF WORKSHOP TIME TABLE.jpg

TEF WORKSHOP TIME TABLE 2.jpg

Karibuni.

====

Update ya Matukio

- MC wa event hii ni Innocent Prim Mungi, amemkaribisha Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, TEF, Deodatus Balile, kutoa neno la ukaribisho, kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkila.

- Balile ameitambulisha TEF, ina wanachama 180, amempongeza Innocent Mungy, kila anaposhika, taasisi hiyo huwa inaonekana, pia amempongeza na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkilia kuhutubia.

- Mkurugenzi Mkuu wa PDCP, Dr. Emmanuel Mkilia anazungumza kwa kutoa a keynote address

HOTUBA YA DKT. EMMANUEL LAMECK MKILIA, MKURUGENZI MKUU WA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI (PDPC) KATIKA KUFUNGA WARSHA YA DHANA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KWA JUKWAA LA WAHARIRI KATIKA HOTELI YA MORENA, MOROGORO – TAREHE 1 MACHI 2025

Bwana Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania; Bi. Anita Mendoza, Kaimu Mtendaji Mkuu pamoja na Menejimenti ya Jukwaa la Wahariri Tanzania; Menejimenti ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mlioko Hapa; Ndugu Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari na Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania; Watoa Mada Mliotoa mada Mbalimbali Katika Warsha Hii; Ndugu Zangu Waandishi wa Habari Mliopo Hapa; Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana; Nawasalimu Kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Habari za mchana huu. Ni matumaini yangu kuwa tumekuwa na siku nzuri.

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kushiriki katika warsha hii muhimu kuhusu Faragha na Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Jukwaa la Wahariri hapa Morogoro.

Pia, napenda kutoa shukrani za dhati kwa wote walioshiriki kuandaa warsha hii kutoka Jukwaa la Wahariri pamoja na kutoka kwenye Tume (PDPC), Wahariri wote mlioshiriki, na kwa michango yenu ya kina katika mijadala ambayo imetuwezesha kuelewa kwa kina masuala ya ulinzi wa taarifa binafsi na wajibu wa vyombo vya habari katika kuhakikisha kuwa faragha ya wananchi inalindwa, hasa katika zama hizi za uchumi wa kidijitali.

Ndugu Mwenyekiti na Washiriki;Tangu kufunguliwa kwa warsha hii pale asubuhi, tumepata fursa ya kupitia mada muhimu ambazo zimejikita katika dhima kuu ya faragha na ulinzi wa taarifa binafsi. Baadhi ya mada zilizowasilishwa zilijikita katika maeneo kadha ikiwemo: Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Safari ya utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa taarifa Binafsi Tanzania – tumeona safari ya nchi yetu katika suala zima la faragha na dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi, tulikotoka na tulipo sasa hivi, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa ulinzi wa taarifa binafsi katika uchumi wa kidijitali unaotekelezwa nchini.

Utangulizi na Wajibu wa Tume na Ufafanuzi kuhusu Taarifa Binafsi

Tumeweza kuelimishwa na kufahamu majukumu ya Tume na wajibu wake pamoja na kuweza kufahamu hasa taarifa binafsi ni zipi na madhara ya taarifa hizo zikifika kwenye mikono ambayo haiko salama. Lakini pia tumeona chamngamoto za utekelezaji wa Sheria pamoja na njia za kukabiliana na changamoto hizo.Misingi ya Kisheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini Tanzania

Ambapo tumejifunza kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na. 11 ya 2022 na Kanuni zake, ikiwa ni pamoja na wajibu wa vyombo vya habari katika kuheshimu faragha na taarifa binafsi za watu wanaporipoti habari mbalimbali zinazohusu taarifa binafsi za watu.Wajibu wa Vyombo vya Habari Katika Ulinzi wa Faragha za Watu – katika suala hili tumeona umuhimu wa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kuhakikisha kuwa taarifa binafsi za watu haziwekwi hadharani bila ridhaa yao au bila uhalali wa kisheria hususani heria zinazosimamia Sekta ya Habari na Mawasiliano nchini huku ikizingatiwa umuhimu wa haki ya wananchi kupata habari.Tumeelezwa hapa Athari za ukuwaji wa Teknolojia Zinazoibukia na Uvunjifu wa Faragha katika Maisha ya Kijamii na Uchumi wa Kidijitali

Tumeshuhudia mifano hai ya jinsi ukiukwaji wa faragha unavyoweza kuathiri maisha ya mtu binafsi, biashara na hata taasisi za umma na binafsi na hususani kwenye Vyombo vya habari kutokana na kukua kwa teknolojia.Jukumu la Jukwaa la Wahariri na Vyombo vya Habari katika Kusaidia Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Hii imeibua hoja muhimu kuhusu jinsi wahariri na wanahabari wanavyoweza kushirikiana na Tume kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheria hii unakuwa wa ufanisi.

Ndugu Mwenyekiti na Washiriki;Kutokana na mijadala iliyojitokeza katika Warsha na mafunzo haya, ni dhahiri kuwa tunahitaji hatua za pamoja kati ya Tume (PDPC) na Jukwaa la Wahariri ili kuimarisha faragha na ulinzi wa taarifa binafsi kwa manufaa ya jamii yetu.

Hivyo basi, tunapohitimisha warsha hii, Tume inapendekeza yafuatayo:

Ushirikiano wa karibu kati ya Tume na Jukwaa la Wahariri ili kuhakikisha kuwa elimu juu ya ulinzi wa taarifa binafsi inafika kwa wanahabari wote na inajumuishwa katika Sera na Maadili ya vyombo vya habari. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa Vyombo vya Habari vinajisajili Tume na kuwa na Maafisa wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kuonesha kwa jamii ya Kimataifa, Kikanda na hapa nchini kuwa Vyombo vya Habari vya Tanzania vinazingatia faragha na ulinzi wa taarifa binafsi.

Tume na Jukwaa la Wahariri Kuandaa Mwongozo wa Vyombo vya Habari kuhusu Ulinzi wa Faragha na Taarifa Binafsi – Mwongozo huu utasaidia kutoa mwangaza wa kimaadili na kisheria katika uandishi wa habari ili kuzuia uvunjaji wa haki za faragha za watu na hivyo kulinda faragha hizo na taarifa binafsi kwa mujibu wa Sheria bila kuingilia Uhuru wa Vyombo vya Habari na haki ya wananchi kupata habari.Kuendelea na mafunzo ya mara kwa mara kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi na kanuni zake ili kuboresha uelewa wa dhana hii muhimu.

Hili ni jambo muhimu na tukishirikiana elimu hii itawafikia waandishi wote wa habari nchini na kuifanya Tanzania kuwa sehemu ya kuiga katika kulinda faragha na ulinzi wa taarifa binafsi.Kuanzisha dawati la kushughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa faragha ndani ya vyombo vya habari

Hili litasaidia kuhakikisha kuwa malalamiko yanayohusiana na uvunjifu wa faragha yanashughulikiwa kwa haraka na kwa haki ndani ya vyombo vya habari, vyama vya wanahabari na taasisi zote zinazofanya kazi kuhakikisha Sekta ya Habari na Mawasiliano kwa Umma inakuwa kinara wa kusimamia haki za faragha na ulinzi wa taarifa binafsi.Kufanya tafiti za pamoja kati ya Tume na Jukwaa la wahariri pamoja na Taasisi za Kihabari nchini na Vyombo vya Habari ili kuelewa changamoto zinazoikumba Sekta ya Habari katika kutekeleza wajibu wake wa kulinda faragha za watu na taarifa binafsi na kupendekeza suluhisho sahihi kwa Sekta ya Habari bila kuathiri majukumu na matakwa ya Sheria na kanuni za Sekta ya Habari nchini.

Ndugu Mwenyekiti na Washiriki Katika kuzindua rasmi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi tarehe 3 Aprili 2024, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliweka bayana dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha kuwa haki ya faragha inalindwa kwa mujibu wa sheria. Alisisitiza kuwa ushirikiano wa wadau wote, hususan Vyombo vya Habari, ni muhimu ili kutekeleza sheria hii kwa ufanisi. Hivyo basi, tunawaomba Wahariri na Wanahabari wote nchini kuendelea kushirikiana nasi kwa karibu ili kutekeleza jukumu hili kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Tangu kuanzishwa kwa Tume mmekuwa sehemu muhimu ya kuiwezesha Tume kutoa elimu kwa umma na kuripoti vizuri taarifa kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Tume inawashukuru sana

Ndugu Mwenyekiti na Washiriki;.Nina imani kuwa warsha hii imekuwa yenye manufaa makubwa na itakuwa chachu ya utekelezaji wa mabadiliko tunayoyahitaji katika ulinzi wa faragha na taarifa binafsi. Ni matarajio yangu kuwa kila mmoja wetu ataendelea kuwa balozi wa ulinzi wa faragha na taarifa binafsi kwa kuhakikisha kuwa tunazingatia sheria na maadili katika utendaji wetu wa kila siku.

Kwa haya machache, natoa shukrani kwa wote waliofanikisha warsha hii na natangaza kuwa warsha hii imefungwa rasmi. Niwatakie safari njema mnaporejea kwenye sehumu zenu za kazi. Mungu awabariki sana.

Paskali
 
Wanabodi

Niko hapa Morena Hotel Morogoro kuwaletea live, warsha ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Jukwaa la Wahariri (TEF) kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Karibuni.

====

Update ya Matukio

MC wa event hii ni Innocent Prim Mungi, amemkaribisha Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, TEF, Deodatus Balile, kutoa neno la ukaribisho, kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkila.

P.
Sawa sawa P,
 
Mkurugenzi mkuu amesema, kwa mujibu wa ibara ya 16 ya katiba, kila mtu anastahili faragha, na faragha hiyo, inapaswa kulindwa kwa gharama yoyote.
P
 
Ujio wa mapinduzi ya kidigitali, ukijisajili kwenye digital media yoyote, unakuwa umetumia taarifa zako bifnafsi, bila taarifa hizi kulindwa, zinaweza kutumika vibaya.
P
 
Baada ya makaribisho rasmi, ya Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkilia, sasa inawasilishwa mada ya kwanza, ya Data Protection na faida za data protection, inayowasilishwa na Eng. Stephen Wangwe.
P
 
Wanabodi

Niko hapa Morena Hotel Morogoro kuwaletea live, warsha ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Jukwaa la Wahariri (TEF) kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Karibuni.

====

Update ya Matukio

- MC wa event hii ni Innocent Prim Mungi, amemkaribisha Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, TEF, Deodatus Balile, kutoa neno la ukaribisho, kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkila.

- Balile ameitambulisha TEF, ina wanachama 180, amempongeza Innocent Mungy, kila anaposhika, taasisi hiyo huwa inaonekana, pia amempongeza na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkilia kuhutubia.

- Mkurugenzi Mkuu wa PDCP, Dr. Emmanuel Mkilia anazungumza kwa kutoa a keynote address

P
Tunaomba Ufafanuzi kuhusu watu wasiojulikana ambao kumbe wengine hawatakiwi wajulikane

Je jamii haitakiwi kuwajua hao watu ambao wanajulikana ila hawatakiwi wajulikane

Tunaomba maelekezo yanayo jitoshereza kuhusu watu wasiojulikana ambao hawatakiwi wajulikane

Bila maelezo yanayo jitoshereza nadhani jamii itkuwa inachukua sheria mkononi
 
Wanabodi

Niko hapa Morena Hotel Morogoro kuwaletea live, warsha ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Jukwaa la Wahariri (TEF) kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Karibuni.

====

Update ya Matukio

- MC wa event hii ni Innocent Prim Mungi, amemkaribisha Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, TEF, Deodatus Balile, kutoa neno la ukaribisho, kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkila.

- Balile ameitambulisha TEF, ina wanachama 180, amempongeza Innocent Mungy, kila anaposhika, taasisi hiyo huwa inaonekana, pia amempongeza na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dr. Emmanuel Mkilia kuhutubia.

- Mkurugenzi Mkuu wa PDCP, Dr. Emmanuel Mkilia anazungumza kwa kutoa a keynote address

P
Mkuu, usiache kupita Chipukizi au Kahumba, utanishukuru
 
Saa hizi ni mada ya III inawasilishwa, ni mada ya legal and regulatory framework, inayowasilishwa na Adv. Humphrey Mtuy.
P
 
Mada ya mwisho ni Emerging Technology na changamoto za data protection, ikiwemo ujio wa akili mnemba, AI., inayowasilishwa na Dr. Noe Nnko.
P
 
Back
Top Bottom