Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni. Hii town ya wajanja, vijana wanaojua kuvaa, wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji... Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa. Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni. Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock garden. Mitaa maarufu ya kihuni kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.
Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka. Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki.. Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa kuitwa Ya mungu ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini. Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.
Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill. Hapa kuna mtu anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu. Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha kazi Dj Peter Moe.
Watu wa Moro najua mpo wengi humu JFnaomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.
Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk
Unaikumbuka Miss Morogoro? Unamkumbuka Alex Nictas?
Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk
Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu kina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos nk
Unakumbuka wagiriki na bata zao kwa Mama Perina na Acropol? Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?
Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona DStv bure.
Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakara na kikundi?
Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan cinema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden?
Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu KG & Forest?
Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu?
Unamkumbuka Ndanje jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?
Unamkumbuka tozi wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi? Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze domp?
Unamkumbuka Achimpota? Unaikumbuka bus la Chambo?
Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauzi na Ulaya?
Umeishi mtaa gani Mafisa, Msufini, Kilakara, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?
Kuna watu maarufu wengi sana DSM ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town. Hakika Morogoro ni jiji kasoro bahari.