Moja ni bora kuliko sifuri

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,229
MOJA NI BORA KULIKO SIFURI

Watu wengi wamekuwa wakiweka mipango mizuri na mikubwa sana kwenye maisha yao. Ila katika utekelezaji hujikuta wanakwama.
Chanzo kikubwa cha kukwama huwa ni kutaka kufanya mambo hayo yote makubwa kwa wakati mmoja au kwa muda mfupi.

Lakini haijawahi kutokea sehemu yoyote kwenye maisha yetu mambo yakaenda haraka kama tunavyotarajia. Kila kitu kinahitaji muda.

Sasa leo nataka nikushirikishe mbinu ambayo itakusaidia kuanza safari yako ya kufikia mipango mikubwa uliyojiwekea bila ya kukata tamaa.
Mbinu hiyo ni kuwa na dhana kwamba MOJA NI BORA KULIKO SIFURI.

Ndio moja ni bora kuliko sifuri kwenye namba, na hata kwenye maisha hali iko hivyo hivyo.
Unataka kuanza biashara kubwa sana, lakini huwezi kuanzia juu, anza na mteja mmoja, ni bora kuliko kusubiri.

Ukishapata mteja mmoja endelea kuongeza mwingine mmoja na mmoja tena na tena na tena. Hii ni bora kuliko kutokufanya chochote kwa kusubiri mambo yawe mazuri.

Unataka kuandika kitabu, huwezi kuandika chote ndani ya siku moja.

Anza na dhana kwamba moja ni bora kuliko sifuri.
Na kila siku andika sura moja ya kitabu.

Kama sura moja ni ndefu sana andika ukurasa mmoja, kisha endelea kuongeza moja kila siku. Itafika siku kitabu kitakuwa kimekamilika.

Unataka kuanza kufanya mazoezi, huwezi kuanza kwa kukimbia kilometa moja au zaidi ya hapo. Utachoka na kukata tamaa.

Lakini unaweza kuanza na kutembea hatua chache, au kupiga push up chache, au kuruka kamba.
Moja ni bora zaidi ya sifuri.
 
hiyo ni principle juu sana katika maisha,kila kitu unachohitaji katika maisha yako ni muhimu sana lakini huwezi kupata vyote kwa pamoja,so lazima kimoja kitangulie kabla ya kingine kufuata.mfano unahitaji gari,nyumba,mke/Mme bomba etc,lazima uanze na kimoja then kingine then kingine
 
Asante kwa maoni.
 
Asante kwa kusoma.
 
Asante kwa maoni yako mazuri.
 
Aisee kweli mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…