the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 491
- 695
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Ali Kawaida, amesema kuwa vyama vya upinzani havina maandalizi wala ushawishi wa kushindana na wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2025, akidai kuwa vinatafuta sababu za kujiondoa kwenye mchakato huo.
Akizungumza Jumatatu, Machi 17, 2025, jijini Dodoma, Kawaida amesema wapinzani hawawezi kuhimili ushindani dhidi ya mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ally Mwinyi kwa upande wa Zanzibar. Amesisitiza kuwa kauli ya wapinzani ya "no reform, no election" haitaizuia CCM kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kawaida ametoa kauli hiyo baada ya kuzindua nyumba ya mtumishi wa UVCCM iliyojengwa na umoja huo katika mkoa wa Dodoma, eneo la Iyumbu.