Pre GE2025 Mohamed Kawaida: Ajenda ya mitano tena ni kwa Rais Samia na Rais Mwinyi tu. Vijana twende tukagombee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
782
958
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewatoa hofu vijana ambao wanataka kuwania nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kuwa wakae tayari kuwani nafasi hizo kwakuwa ajenda ya Mitano Tena ni kwa Mgombea wa Urais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea wa Urais Mteule wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Kawaida amesema hayo leo tarehe 17 Februari, 2025 wakati akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Chuo cha UVCCM cha Tunguu alipoenda kuweka jiwe la msingi.

"Kumezuka tabia kwa Wawakilishi, Wabunge, ajenda ya mitano tena ilikuwa ya wawili tu Mwenyekiti wetu wa CCM na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar. Wasiwatishe vijana kuwa wao mitano tena, vijana nendeni mkagombee," amesisitiza Ndg. Kawaida


Soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
20250211_191743.jpg
 
Back
Top Bottom