Louis II
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 3,030
- 4,647
Assalaam Aleiqum wapendwa,
Niwe muwazi tu kwamba, miye si mpenzi/mfuasi wa siasa za Rais J.P Magufuli kwani kila mtu anafahamu hali halisi ya kisiasa ilivyo kwa sasa hapa nchini kwetu.
Chini ya uongozi wa rais JPM, hali ya kisiasa imekuwa mbaya hasa kwa upande wa upinzani kwani wanachukuliwa (considered) kama Wahaini (wanatumwa na mabeberu). Chini ya utawala wa Awamu ya tano, weaknesses zimekuwa nyingi na zimekuwa kama wimbo wa taifa maana zipo kila uchwao na hakuna Positive solution/action/change yoyote Inayochukuliwa. Kifupi sitataja madhaifu yote ya awamu hii ya tano Katika utawala wake kwa sababu mengi yanajulikana na yanasemwa kila siku humu na huko uraiani kuhusu "Tyrannic leadership" ya Mh. JPM.
Lakini Kama tittle ya Uzi hapo juu inavyojieleza "Mnyonge Mnyongeni Haki yake mpeni", kwa kweli Serikali hii kwenye suala la miundombinu hasa ya barabara imejitahidi sana kuboresha na kuzitengeneza kwa wingi hasa katika maeneo yaliyokuwa yamesahaulika hapo mwanzo. Mfano mzuri kwa hapa Dar ES Salaam, ni Wilaya Za Temeke na Ilala ukijumuisha viunga vyao, kumekuwa na utengenezwaji na uboreshaji wa barabara hasa zile ambazo zilikuwa kero kwa watumiaji kipindi cha Mvua na maeneo mengi yanapitishiwa barabara za lami.
Ushauri: Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi Mazuri ambayo Hayatasahaulika vizazi kwa vizazi mf. SGR, Stiglers Gorge, Kununua ndege n.k. lakini yapaswa Kufanya marekebisho kwenye baadhi ya mapungufu yake ambayo yamekuwa yakiimbwa na Watu wa kaliba zote kila uchwao....Nina imani, serikali hii itakuwa bora zaidi iwapo itafuata utawala Wa sheria unaozingatia maslahi ya taifa kwa manufaa ya jamii yake Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii, Kiitikadi, na Kifikra. Wahaddha Assalaam Aleiqum!