LGE2024 Mnyeti: Hamasishaneni katika familia kupiga kura kesho

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,107
2,652
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo na Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti, amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kesho kupiga kura kama walivyojiandikisha.

Akizungumza katika Kata ya Usagara wakati akifunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Misungwi, Mnyeti amesisitiza umuhimu wa kufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa. Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuondoka kwenye vituo vya kupiga kura baada ya kumaliza ili kuepusha msongamano.

Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Pia, amehimiza wananchi kuhamasishana katika ngazi ya familia na mtaa ili kuhakikisha hakuna anayeacha kupiga kura, kwani ni haki ya kila Mtanzania kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom