Wakuu habari zenu!
Nimekuwa nikifanya mazoezi ya viungo pamoja na kukimbia kwa muda mrefu kama miez 8 hivi,huwa natoka nakimbia kuanzia Mabibo hostel napita Ubungo mataa,gate maji,utawala udsm,ardhi univ,mliman city halafu narudi na Sam Nujoma to Ubungo then hostel.
Sasa wiki mbili zilizopita nilianza kukimbia kawaida lakini nilipofika gate maji misuli nyuma ya magoti ilinishika vibaya sana pia goti la mguu wa kushoto likawa kama lime-dislocate,nilijaribu kuendelea kukimbia lakini misuli ilinishka sana,nikarudi natembea,nikapumzika siku 3 nikajaribu kukimbia hali iko ile ile tena sifiki hata land mark hostel,nikajaribu baada ya wiki,tena hali iko ile ile,nikajaribu tena juzi hali iko vile vile.
Naomba mnisaidie, nimejaribu kutumia dawa za kuchua lakini sipati nafuu,tena hata nikitembea haraka misuli ina tight.
Kama kuna doctor humu au yeyote mwenye kunipa ushauri nawaomba au wakuni connect wa matabibu wa timu za michezo naomba.