Tukusi Tinka Janjuzi
New Member
- Aug 13, 2024
- 1
- 1
Mmomonyoko wa maadili tunaoushuhudia hivi sasa katika jamii na taifa kwa ujumla ni matokeo ya kukiuka asili yetu kama "WANA WA TANZANIA NA WAAFRIKA". Mfano, kwa wale wazaliwa wa miaka ya nyuma kulikuwa na unataratibu wa familia kushiriki mlo wa pamoja, huenda ikawa mchana au jioni, kukaa pamoja kama familia wazee wetu walikuwa na uwezo wa kutambua tabia mbalimbali za watoto na kuzikemea, hasa tabia za utovu wa nidhamu.
Ninafahamu kwa sasa kitu hicho hakiwezekani kutokana wingi wa mambo ya kutafuta riziki kama ujuavyo maisha yanabadilika na mahitaji yanazidi kuongezeka hivyo nguvu na kasi ya utafutaji inaongezeka pia. Mfano huo hapo juu utumike kama kielelezo muhimu kinachotoa tafsiri ya umuhimu wa wa wazazi kutenga muda maalum wa kukaa na watoto wao na kufanya uchunguzi wa tabia mbaya nyemelezi na wazikemee. Hii itasaidia kwa kiasi fulani kuunda vijana bora pamoja na changamato ya uhuru wa kujipakulia tabia zisizofaa katika mitandao ya kijamii.
Kukaa pamoja kama familia kunaongeza upendo na kuondoa hali ya mtoto kujiona kama kiumbe kisicho na mwenyewe hali inayopelekea kutojali hisia zake mwenyewe na mtu mwingine. Vijana wa leo ambao wanaonekana kuwa na roho ngumu ukifuatilia sababu za wao kufikia hali hiyo utagundua kuna sehemu mzazi hakufanya kazi yake ipasavyo.
Kama wasemavyo waneni "Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina yake". Maana yake ni kwamba mtoto hufuata tabia za wazazi wake au watu wazima alionao karibu; kwa muktadha huo ni muhimu wazazi kutenga muda na kukaa na watoto wao. Turejee katika asili japo kwa mbinu za kisasa.