Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,201
- 5,585
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) ikimtaja Matthew Livelsberger, kuwa mtu aliyefariki ndani ya gari aina ya ‘Tesla Cyber truck’ iliyolipuka nje ya hoteli maarufu ya Trump jijini Las Vegas, polisi nao wamesema ni tukio la kujitoa muhanga.
Tukio kilo lilitokea zikiwa zimepita saa chache tangu, tukio lingine la dereva wa gari aina ya Pickup kugonga na kuwaua watu 15 jijini New Orleans nchini Marekani wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
Hata hivyo, FBI wamesema matukio hayo hayana uhusiano.
"Hadi sasa hakuna usahidi kwamba haya matukio yote mawili yana uhusiano wa aina yoyote,” alisema Mkuu wa Kitengo cha FBI jijini Las Vegas FBI, Spencer Evans.
"Hatua za kiuchunguzi na taarifa za ndani ya Jeshi la Marekani zinaonyesha kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la afya ya akili, pia tumebaini kuwa kulikuwa na changamoto za kifamilia zilizokuwa zikimsumbua na kusababisha tatizo hilo,” alisema Evans.
Livelsberger, ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Marekani katika kambi iliyoko Corolado, alikutwa akiwa amefariki ndani ya gari hiyo huku akitajwa kuwa na mgogoro binafsi uliokuwa ukimsumbua.
PIA SOMA
- Gari aina ya Cyber Truck la Elon Musk lalipuka huko Las Vegas Marekani mbele ya jengo la Trump Tower la Donald Trump