Jbst
JF-Expert Member
- Nov 29, 2020
- 1,968
- 4,069
Nanukuu "Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limewataka Wazazi na Walezi wa Vijana kupuuza taarifa za uzushi unaolenga kuwatia hofu Vijana waliopangiwa kuhudhuria Mafunzo ya JKT katika makambi mbalimbali kutokwenda kuripoti makambini, kwa kile kinachodaiwa kuwa eti, mafunzo ya JKT ni mateso, yana unyanyasaji na udhalilishai hususani kwa Vijana wa jinsia ya kike.
JKT imesema taarifa hizo ni uzushi kwani mafunzo hayo ni muhimu sana kwa ustawi wa Vijana na Taifa kwa ujumla “Hivi karibuni JKT ilitoa wito kwa Vijana wote waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2023, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria lakini kumezuka taharuki kubwa katika mitandao ya Kijamii kutoka kwa baadhi ya Watu wenye nia ovu wasilolitakia mema Taifa
letu”
“Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na yale ya Kujitolea yamelenga kumjengea kijana wa kitanzania uzalendo, ukakamavu, nidhamu na kuleta umoja wa kitaifa na yanaendeshwa kwa kuzingatia mila, desturi na tamaduni za kitanzania”
“JKT katika kuhakikisha Vijana hao wanakuwa salama wakati wote, Makambi na Vikosi vote vya JKT vina Baba na Mama Mlezi (Patron a Matron) ambao wamewekwa mahususi ili kusimamia ustawi wa Vijana wa kiume na wa kike kwa kipindi chote wanapokuwa makambini”
Mwisho.
Ningependa kufahamu maisha ya huko ila bahati mbaya sikufanikiwa kufika, wale mliopita JKT tunaomba machache yaliyopo huko.