Mliokuwa mkiomba Mh. Waziri Mkuu Majaliwa Majaliwa atumbuliwe mnajisiaje baada ya kutumbuliwa Dk Bashiru Ally?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
7,495
8,816
Wengi humu humu walitabiri nani angekuwa makamu wa rais wakimtaja hata Dk Bashiru Ally. Wengine walisema wazi waligemea mhe Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa atupwe. Haiwi haiwi huwa. Sijui mnajisikiaje ambao watu wenu wametoswa? Ni swali tu.
 
Bashiru hakutumbuliwa, bali Rais mpya hakutaka kufanya naye kazi, jambo ambalo ni la kawaida sana. Anayetumbuliwa ni yule aliyekosea katika utendaji wake, Bashiru ana mwezi mmoja tu kwenye nafasi hiyo; atakuwa kakosea wapi!
 
Kwani P.M alikuwa na kashfa yoyote,tuliotegemea kutikiswa ni mzee wa jalalani,bashiru,jafo na dotto wa hazina,binafsi naona waziri Mkuu hana impact na hakuwa na impact yoyote kipindi cha magu zaidi ya siasa uchwara na kupokea maagizo kutoka kwa boss wake.Hana sumu pia anaheshima ya hali ya juu kwa boss mpya hivyo atadumu.
 
Bashiru hakutumbuliwa, bali Rais mpya hakutaka kufanya naye kazi, jambo ambalo ni la kawaida sana. Anayetumbuliwa ni yule aliyekosea katika utendaji wake, Bashiru ana mwezi mmoja tu kwenye nafasi hiyo; atakuwa kakosea wapi!
Alikosea kwa kusema hatakubali uteuzi wowote akaishia kuupwakia huku bila aibu akiramba matapishi yake.
 
Je katiba inasemaje na anaipuuza vipi?
...nafasi ya waziri mkuu ilipaswa kuteuliwa upya na kuthibitishwa na bunge, Kisha kuapishwa.Kisha angeapishwa na rais.Hata Kama angemtaka Tena majaliwa angemrudisha Tena.Kisha angeunda Baraza jipya.Mama mwanzo alianza vizuri.Huku anakoelekea kukanyaga kiapo chake, sie wengine tunaoipenda nchi yetu kuliko chochote hatutamuunga mkono kwa hili.Huenda Kuna watu ndani ya serikali au ccm wamemshauri vibaya ili achafuke mapema kwa malengo yao.Binafsi nilitamani Sana apige miaka kumi lakini kwa mwendo huu naanza kuona Shaka.Kulinda kiapo Cha urais ni Jambo la msingi Sana hasa kuitii katiba yetu.
 
Wengi humu humu walitabiri nani angekuwa makamu wa rais wakimtaja hata Dk Bashiru Ally. Wengine walisema wazi waligemea mhe Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa atupwe. Haiwi haiwi huwa. Sijui mnajisikiaje ambao watu wenu wametoswa? Ni swali tu.
Watabiri na wabashiri wamesha fanya kazi yao, na SSH kafanya yake. Game over
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…