Mkuu wa Wilaya Msando apiga marufuku magari ya wagonjwa kuhamishwa kwenye vituo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,181
5,553
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando, amepiga marufuku kwa wakurugenzi kwa kushirikiana na watumishi wa idara ya afya, kuhamisha magari ya wagonjwa kwenye vituo husika na kupeleka sehemu nyingine bila sababu maalum.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hayo leo Machi 9, 2024 katika Kijiji cha Msomera wakati akipokea gari la wagonjwa lililokabidhiwa na mbunge wa Handeni Vijijini (CCM) John Sallu na kusema kuna gari la wagonjwa lilipelekwa hapo ila limehamishwa kwa sababu ambazo hazikujulikana.

Mbunge wa Handeni Vijijini baada ya kukabidhi gari hilo amewapongeza wananchi kutoka Ngorongoro kwa kutetea haki za wenyeji wao na kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali.
 
Back
Top Bottom