Mkuu wa Wailaya ya Maswa na Afisa Uhamiaji Wilaya ya Maswa acheni kunyanyasa raia i.e:WAHA

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Nov 30, 2022
914
994
Habarini,
Leo tena Afisa Uhamiaji kaendeleza unyanyasaji wake kwa maelekezo ya DC wa Maswa kwa kutuma askari wa uhamiaji kwenda kumkamata raia mkazi wa Malampaka Wilaya ya Maswa kwa kile anachodai siyo raia wa Tanzania ingawa chanzo chake ni kuwepo mgogoro wa ardhi baina ya Baraka Kabezi na Diwani wa eneo hilo ambao ulitatuliwa na Mkuu wa Mkoa kwa kuwashitikisha wataalamu wa ardhi wa H/Wilaya ya Maswa.

Hivi kuna weledi kweli ndani ya Jeshi la Uhamiaji la Tanzanaia iwapo raia anamiliki kitambulisho cha NIDA,cheti cha kuzaliwa,kitambulisho cha kupigia kura na uhamiaji wakabariki kwa kupitisha fomu ya nida na kugonga mihuri,mtu kapiga kura zaidi ya mara 3,kazaliwa hapa,kasoma shule na kuajiriwa serikalini pamoja na wazazi wake hadi kustafu,leo anaambiwa siyo raia na kila mara anasumbuliwa kwa kukamatwa na kutelekezwa kwa gharama zake kitu ambacho ni uonevu hasa.

Viongozi husika lioneni hili raia wananyanyaswa na idara ya uhamiaji na kuingizwa hasara na gharama zisizo za lazima basi kama ni hivyo WAHA wote URAIA wao UBATILISHWE au waoneshwe nchi yao ni ipi siyo kusumbuana.

Nawasilisha.
 

Attachments

  • IMG-20240611-WA0004.jpg
    IMG-20240611-WA0004.jpg
    33.9 KB · Views: 12
Back
Top Bottom