Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,724
- 4,475
Wakuu,
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, ameonya vikali baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Ushetu waliogeuka kuwa mawakala wa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge, akisema ataagiza wafukuzwe kazi ili kuepusha kuchanganya siasa na kazi za serikali.
Macha alitoa onyo hilo jana katika Kata ya Kisuke alipokuwa kwenye ziara ya kukagua hali ya uzalishaji wa zao la pamba na kusikiliza changamoto za wakulima.
Alibainisha kuwa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wameacha majukumu yao na badala yake wanashiriki katika siasa kwa kuwatafutia kura wagombea wa nafasi mbalimbali, jambo ambalo halikubaliki. Alisisitiza kuwa hatasita kuiwasilisha orodha ya watumishi hao kwa Mkuu wa Wilaya ili hatua zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.
"Nina orodha ya baadhi yao ambao badala ya kufanya kazi walizotumwa na serikali, wamegeuka kuwa wanasiasa. Nitaikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ili ichunguzwe, na wale watakaobainika tutaagiza mamlaka husika ziwafute kazi ili waendelee na siasa zao huko," alisema Macha