Nimefadhaishwa na taarifa ya habari ya Star TV leo kuwa mkuu wa mkoa Shinyanga kamfukuza kazi mtendaji halmashauri ya Kahama heti kwa kuongoza vibaya msafara wa mkuu wa mkoa alipotembelea wilaya ya Kahama na kutaka kussababisha ajali,mimi namuomba waziri mkuu atoe muongozo wa aina ya majipu kwa watendaji wake,haiwezekani mtumishi wa serikali asiye traffick polisi asimamishwe kazi heti hakuongoza msafara wa mkuu wa mkoa vizuri.
Hivi who is mkuu wa mkoa hadi a deserve motorcade ya aina yake?je huyo aliyesimamishwa, kazi ya kuongoza magari ni TOR ya ajira yake serikalini yake,je amewahi kupelekwa NIT kusomea VIP Motorcade au hiyo taaluma ya kuongoza misafara ya wakuu wa mikoa na ma-DC anategemewa kuwa aliipata wapi?
Kama usipotolewa muongozo watu wengi wataumia sana kwa baadhi ya viongozi wanaodhani kufukuza watu kazi ndio sera kuu ya awamu ya tano