Mkuu wa Mkoa feki wa Dar Es Salaam akamatwa kwa utapeli

KingKacha

Senior Member
Jun 15, 2016
118
119
POLISI YAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA TUHUMA ZA KUTAPELI KUTUMIA JINA LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.

JESHI la Polisi Mkoa Ilala linamshikilia mkazi wa Pugu, Imarock Paula Rutashabya ‘ Issa Mohamed Jiunga’ kwa tuhuma za kutumia jina la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kujipatia kipato kwa kupiga simu kwa watu wenye nafasi zao kwa kuomba fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema tukio hilo lilitokea Juni 16 mwaka huu maeneo ya mtaa wa Samora Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kamanda, Hamduni amesema mtu alikamatwa baada ya kumpigia simu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jones Logistics LTD , James Rodrick Luponda na kujitambulisha kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam lengo la kumsaidia kijana wake aliyepata ufadhili wa kusoma lakini anahitaji achangie asilimia 30 sawa na dola za Kimarekani 35,000 ya gharama za chuo kilichoko nchini Ufilipino baada ya kupata ufadhili wa asilimia 70.

Amesema mtuhumiwa katika maongezi yake alimueleza mkurugenzi huyo kuwa fedha hizo atumie benki ya Eco akaunti Kenya au kutoa pesa taslim kwa kumpa namba za simu 0717 338 473 ya kijana anayehitaji msaada kuwa atafika ofisini kwake baada masaa mawili akiwa na nyara zote za fursa ya hayo masomo pamoja na akaunti namba ya benki alizozitaja.
Mtuhumiwa alikamatwa na anahojiwa ili kuweza kupata mtandao wake ambao wanatumia majina ya viongozi kujipatia kipato.

Majina ya viongozi ambayo yanatumika kwa watu kujipatia kipato kwa njia ya utapeli ni Waziri Mkuu , Mkuu wa Mkoa na wengine na kuahidi wananchi kutoa ushirikiano dhidi ya watu wanaotumia majina hayo.
 
Weka picha
 
http://www.https://jamii.app/JFUserGuide/2016/06/polisi-mkoa-wa-ilala-yakamata-matapeli.html
 
http://www.https://jamii.app/JFUserGuide/2016/06/polisi-mkoa-wa-ilala-yakamata-matapeli.html
 
Yaaan hapo utaona ukatiri unapoanzia kwa sababu sadism is inevitable when the sitution is running
Ataereza ukatiri atakaofanyiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…