Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,835
- 10,362
Kutakua na mkutano mkubwa wa kahawa barani Afrika utakaofanyika tarehe 21–22 Februari 2025 katika Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania.
Mkutano huu unaongozwa na Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkutano una lengo la kuimarisha sekta ya kahawa kwa ajili ya kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wanawake kupitia uzalishaji na matumizi ya kahawa barani Afrika.
Mambo Muhimu yatakayojadiliwa:
✔️ Uwezeshaji wa vijana na wanawake kupitia ajira na ujasiriamali katika sekta ya kahawa
✔️ Upatikanaji wa fedha kwa miradi inayohusiana na kahawa kupitia taasisi za kifedha za Afrika
✔️ Uwekezaji katika viwanda vya usindikaji wa kahawa ili kuongeza thamani ya bidhaa
✔️ Kuendeleza biashara ya kahawa ndani ya Afrika kupitia viwango na sera bora
✔️ Kuanzisha Dar es Salaam Declaration kwa ajili ya kuhamasisha Muungano wa Afrika (AU) kusaidia sekta ya kahawa
Mkutano huu utahudhuriwa na viongozi wa nchi, mawaziri, wakuu wa mamlaka za kahawa, wawakilishi wa sekta binafsi (wakulima, wauzaji wa kahawa, wasindikaji), na wadau muhimu wa sekta ya kahawa.
Mkutano huo kwa siku ya tarehe 21 February 2025 uta hudhuriwa na mawaziri wa kilimo wa nchi hizo na tarehe 22 February 2025 utahudhuriwa na wakuu wa nchi wa mataifa ya Afrika huku zaidi ya washiriki 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajia kuhudhuria.
✅ Tarehe: 21–22 Februari 2025
✅ Mahali: Julius Nyerere International Convention Centre, Dar es Salaam, Tanzania
FUATILIA LIVE:
View: https://www.youtube.com/live/g5djiMf20HY?si=9JV2vTK9WBrKcyKu