Mkurugenzi wa Halotel na wenzake 5, wahukumiwa kulipa faini ya milioni 24 au kwenda jela mwaka mmoja. Halotel yalipa Bil 30

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,969
13,743


MKURUGENZI wa Halotel, Son Nguyen(46) na vigogo watano wa Kampuni ya Viettel Tanzania, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), kwa ajili ya kukiri makosa yao 10 likiwemo la kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), hasara zaidi ya bilioni 75.

Wakili wa utetezi Benedict Ishabakaki, alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa kutajwa.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai shauri lilipelekwa kwa kutajwa ambapo upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya kudai hayo, Wakili wa utetezi Ishabakaki, alidai wateja wake tayari walishaandika barua kwa DPP, ambapo bado wanaendelea na mazungumzo.

" Wateja wangu wameandika barua kwenda ofisi ya DPP kwa ajili ya kukiri makosa yao, ambapo wanaendelea na mazungumzo, hivyo tunaomba tarehe fupi," alidai.

Akijibu hoja hizo, Wakili Wankyo, alidai kwa kuwa wanaendelea na mazungumzo ni wajibu wa Wakili wa utetezi kufuatilia mazungumzo hayo yalikofikia na yakiwa tayari wataiambia Mahakama.

Hakimu Simba, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya siku ambayo watapangiwa kuletwa itatolewa hati ya kuletwa washitakiwa hao Mahakamani, kesi iliahirishwa hadi Julai 22, mwaka huu kwa kutajwa na washitakiwa walirudishwa rumande.

Mbali na Nguyen washitakiwa wengine ni Nguyen Minh (40) na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel.

Inadaiwa washitakiwa hao walitenda kosa kati ya Juni 8, mwaka 2017 na Machi 26, mwaka huu maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida.

Ilidaiwa kati ya Juni 8, mwaka 2017 na Machi 26,mwaka huu maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA.

Pia alidai kati ya Julai 7, mwaka 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu.

Katika mashitaka la nne, inadaiwa washitakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganisha Viettel Tanzania na Vietnam kinyume na sheria.

Vile vile Juni 8, mwaka 2017 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya sh. bilioni 75.

Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, mwaka 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya sh. bilioni 3.03.

Katika mashitaka ya saba washitakiwa wote wanadaiwa kutakatisha sh. bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu.

Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, mwaka 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha sh. bilioni 3.03 na mashitaka ya tisa na 10, washitakiwa wote wanadaiwa kutakatisha sh. bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.

====

UPDATES: 18:00HRS

=====

1.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu wafanyakazi watano na Kampuni ya Halotel kulipa faini ya milioni 24 au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja

Pia mahakama imehukumu Kampuni ya Halotel kulipa fidia ya sh. bilioni 30 ya kuisababishia Serikali hasara ambapo fidia hiyo imeamuriwa kulipwa ndani ya mwaka mmoja

Vile vile washtakiwa hao katika makubaliano na DPP tayari wamelipa fidia ya sh. bilioni 12

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba

====

UPDATE 2: 19:00HRS

=====

Wamefanikiwa kulipa hiyo faini ya milioni 24.
 

Attachments

  • Halotel charge sheet.pdf
    682.1 KB · Views: 12
Huyu bwana hata kuzimu hawezi kwenda kwa huu utakatishaji pesa wake
Kweli kabisa! Na atakwenda peponi kwa kutakatisha pesa na kuirudisha kwa wamiliki halali yaani sisi wananchi ! Mitaano tenaaa! Nasema uongo ndugu zangu ???
 
Back
Top Bottom