Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime (Elias Ntirihungwa) ambaye ndiye Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini amewafuta Ukuu wa Shule (Sekondari) na Walimu wakuu (Primary) wote ambao Mhe Esther Matiko Mgombea Ubunge CHADEMA ametembelea Shule zao katika kipindi hiki cha Kampeni.
Hii imekuja baada ya Mgombea wa CCM Michael Kembaki kutembelea Shule hizo na kujikuta katika wakati mgumu wa kuonekana kukosa Kura kutoka kwa Wanafunzi ambao walimtamkia wazi wazi kuwa wanakwenda na Esther Matiko *( MSUBHATI TENA 2020)* na si vinginevyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji amewaita kwenye Kikao Walimu wote hao na baadhi ya watumishi wa Serikali jana 02/10/2020 na kuanza kuwatisha na kuwatamkia kuanzia wakati huo hawatambui Kama wakuu wa Shule na Walimu wakuu wasubili maelekezo mengine yanayofuata!
Zaidi Mkurugenzi huyo (Eliash Ntirihungwa) amewaamuru baadhi ya walimu kuandika barua za kutoa maelezo kuhusu ugeni wa Mhe Esther Matiko kwenye Shule zao na kuwalazimisha kuandika baadhi ya maneno kwenye maelezo yao kwa manufaa yake mwenyewe.
Walimu hao wameonekana kuchukizwa na kukerwa na kitendo hicho cha Mkurugenzi (Elias Ntirihungwa) ambaye ndiye Msimamizi wa uchaguzi Jimbo kuwaita na kuanza kuwafokea na kuwadharilisha hasa akijikita kumsema vibaya Mhe Esther Matiko.
Walimu wamechukizwa sana kwani bila upendeleo wameshampokea na kumkaribisha tena Mgombea Ubunge wa CCM (Michael Kembaki) kwenye Shule zao na kumpa nafasi ya kuzungumza na Walimu pamoja na wanafunzi kwa nyakati tofauti na ata Mgombea huyo kutoa baadhi ya vitu kwa Walimu na wanafunzi zikiwemo fedha, Ng'ombe kwa ajili ya wanafunzi kuchinjiwa na ata Mchele mfano Shule ya Sekondari Bomani, Nkende, Rebu na Nyandoto ambapo ni kinyume na Maadili ya uchaguzi 2020. Kwani kufanya hivyo ni kutoa *Rushwa*
Mkurugenzi huyo ameagiza pia Walimu wote ambao wameomba kuwa Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ambao Mhe Esther Matiko ametembelea Shule zao waondolewe kwenye orodha ya watakaoteuliwa kusimamia vituo vya kupigia kura.
Taarifa zinaonesha kuwa Majina yote ya waliomba kusimamia vituo vya kupigia kura Jimbo la Tarime Mjini yanatakiwa kupelekwa Ofisi za CCM Wilaya ya Tarime kwa ajili ya kufanyiwa mchujo kwa kuteua Wasimamizi waliomakada wa CCM ikiwa ni Mkakati wa kukitafutia CCM ushindi wa Mezani.
Sisi Wanatarime Mjini tunapenda kumwambia na kumkumbusha Mkurugenzi wa Mji wa Tarime ambaye ndiye Msimamizi wa uchaguzi Jimbo, hakuna Jambo ambalo hatulijui wakati wote wa kupanga na kutekeleza muhimu zaidi ajiandae Kisaikolojia kwa kuheshimu maamuzi ya Wanatarime Mjini watakayofanya 28/10/2020 na sio kujiandaa kupindua meza siku hiyo.