informer 06
Member
- May 11, 2024
- 55
- 33
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge amesema kuwa Watu zaidi ya elfu 18 kitika kipindi cha mwaka mmoja wamenufaika na huduma mbalimbali za kibingwa kwa magonjwa ya moyo ikiwemo kufanyiwa vipimo bure kupitia utaratibu wa tiba Mkoba kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (Outreach Services ).
Akizungumza Desemba 21, 2024 wakati wataalamu kutoka JKCI wakitoa huduma za tiba Mkoba kwa Wasanii kwenye Kliniki ya JKCI iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health Plaza jijini Dar es Salaam amesema kuwa wasanii ni miongoni kundi muhimu ambalo linaweza kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya huduma hizo ambazo utolewa bure.
Zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano na Bodi ya Filamu Tanzania na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuwafikishia huduma za kibingwa wasanii ndani ya miezi hadi kufikia mwisho wa mwezi Januari 2025.
"Wasanii wamekuwa kioo katika jamii yetu, tukaona ni wakati sasa kuwatumia ili waweze kutusaidia kuielimisha jamii namna ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo kwani magonjwa haya yamekuwa yakichangia vifo vingi duniani"alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema wasanii wanapoyaelewa magonjwa hayo inasaidia kufikisha jumbe kwa jamii kupitia njia mbalimbali za sanaa ikiwemo maigizo,muziki na sanaa nyinginezo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Gervas Kasiga alisema limekuwa jambo la kipekee mwaka huu wasanii kufunga mwaka wakiwa wamefanya uchunguzi wa afya zao na kupata elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Dkt. Gervas aliwataka wasanii kutumia fursa hiyo kwa umuhim kwani nafasi kama hiyo huwa haijitokezi mara nyingi hivyo pale inapojitokeza inapaswa kutumiwa vizuri na kwa maslahi binafsi.
"Kupitia upimaji huu unaotolewa kwa wasanii itatusaidia katika tasnia kujua afya zetu ili tunavyoenda kufanya kazi zetu tuweze kuzifanya kwa ubora kufikia matarajio yetu na matarajio ya nchi yetu", alisema Dkt. Gervas
Aidha msanii wa bongo movie, Steven Mengele amewahasa wananchi kutumia fursa hiyo kufanya vipimo na kufahamu afya zao, ambapo amedai kuwa huduma hizo za kibingwa zinazotolewa bure kama zingekuwa zinalipiwa pesa uenda kuna kundi kubwa lingekosa kuhudumiwa.
Huduma hizo zinatolewa kwa siku za Jumamosi na jumapili kwa wasanii kwenye Kliniki ya Kawe, ambapo fursa hiyo kwa wasanii itahitimishwa mwishoni mwa January 2025.
Itakumbukwa huduma za tiba Mkoba zimekuwa zilitolewa na taasisi hiyo kwa kuwafikia wananchi walipo katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wataalamu bingwa wa masuala ya moyo na lishe wamekuwa wakiweka kambi katika maeneo tofauti na kutoa huduma za kibingwa, kwa mujibu wa Dkt. Kisengi ni kwamba tayari wamefika kwenye mikoa takribani 17