GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,822
- 9,656
Kuna minong'ono imekuwa ikiendelea kwa siku kadhaa sasa kumuhusu RC wa Arusha, Paul Makonda, kwamba anaumwa sana na amekimbizwa South Afrika kwa matibabu. Hisia za baadhi ya watu ni kuwa kalishwa sumu kutokana na kuhatarisha maslahi ya "mafisadi" fulani.
Kwa kipindi chote tokea hizo tetesi zianze, Serikali ya mkoa husika imekuwa kimya. Haijakanusha wala kukubali.
Kulikoni hivyo?
1. Labda Makonda yupo likizo, hivyo hawawezi kusema kwa kuwa hayupo ofisini?
2. Viongozi waandamizi wa mkoa wa Arusha hawajazipata hizo tetesi?
3. Ni jambo zito sana ambalo hawawezi kulielezea kwa umma wakaeleweka?
4. Ni mwendelezo wa tabia zilizozoeleka kwa baadhi ya viongozi wa umma kupenda kudanyanya, kama ilivyotokea kipindi Magufuli alipokuwa mgonjwa?
5. Si utaratibu kwa mkoa kujibu tetesi dhidi ya viongozi wake?