Zama na nyakati zimebadilika......hivyo na vijana wanatakiwa wabadili mitazamo yao katika masuala ya ndoa hasa kwenye nyakati hizi ambazo wanawake na wao ni miongoni mwa wanaotafuta mkate wa kila siku........
Unatakiwa ubadilishe mtazamo kutoka kumchukulia mwanamke kama mama wa nyumbani bali unatakiwa umuone kama mtu anayekusaidia baadhi ya majukumu hapo nyumbani kupitia mshahara wake........
Mtazamo huo utakufanya ujue changamoto na mikiki mikiki anayopitia mkeo akiwa kazini ni kama wewe vile uwapo kazini.....hivyo kupambana na changamoto hizo ili maisha yaendelee kunahitaji jitihada na uvumilivu wa hali ya juu......
Inawezekana mkeo wala hajakudharau bali ni wewe umegoma kubadilisha mtazamo wako juu yake na umeshindwa kuenenda saawa na mabadiliko yake........
Inawezekana umekuwa mkali katika mambo ya kijinga na yeye ameamua kukaa kimya kwa heshima yako kama mume
Inawezekana hata wewe ulikuwa unamnyanyasa na kumsimanga zamani akiwa hana kipato na sasa umeshikwa na wivu kuona kuwa mambo mengi aliyokuwa anakusumbua ana yamaliza mwenyewe kwa mshahara wake......
Suluhu pekee la tatizo lako ni wewe kubadili mtazamo wako juu yake na kuongea naye......huyo ni mkeo ni rafiki yako....mwandani wako....msiri wako na wala sio adui yako......
Vunja ukimya sema naye.....