mandela1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2013
- 837
- 601
Wandugu poleni na majukumu ya kila siku
Wapwa, niko kwenye ndoa mwaka wa tano sasa. Nashindwa kuelewa haya maisha ya ndoa yana uhusiano gani na ya mahusiano kipindi bado hatuna watoto.
Kweli kipindi sina mtoto niko kwenye mahusiano mwenzangu alinipenda sana tofauti na sasa tukiwa na watoto. Hivi sasa hataki kusikia stori zangu, ni yeye na wanae tu. Swali kwa wanandoa wenzangu: Je, ni kweli kila mwanamke anapokuwa umezaa upendo wote huelekezwa kwa watoto?
Kama ndio, vipi kuhusu mumeo aliyekuzalisha? Kwani yeye hastahili upendo au ndo tuwe busy kuijenga familia bila upendo pande zote?
Baadhi ya michango
Wapwa, niko kwenye ndoa mwaka wa tano sasa. Nashindwa kuelewa haya maisha ya ndoa yana uhusiano gani na ya mahusiano kipindi bado hatuna watoto.
Kweli kipindi sina mtoto niko kwenye mahusiano mwenzangu alinipenda sana tofauti na sasa tukiwa na watoto. Hivi sasa hataki kusikia stori zangu, ni yeye na wanae tu. Swali kwa wanandoa wenzangu: Je, ni kweli kila mwanamke anapokuwa umezaa upendo wote huelekezwa kwa watoto?
Kama ndio, vipi kuhusu mumeo aliyekuzalisha? Kwani yeye hastahili upendo au ndo tuwe busy kuijenga familia bila upendo pande zote?
Baadhi ya michango
mandela1, Brother pole Sana, inaonekana unajali Sana familia yako, kitu ambacho ni kizuri. Hili ni tatizo kubwaa Sana kwa wanawake wa siku hizi, japo na uhakika wewe utakuwa ulianza kuzingua kimtindo.
Kiukweli akili za wanawake wanazijuaga wao wenyewe wakati mwingine. Sisi wanaume tuko kwa ajili ya kulinda maslai ya ndoa na familia zaidi kwa ujumla wake, na tunapozumza khs familia, Mara nyingi tuna maanisha baba, mama na watoto, lkn kwa bahati mbaya Sana haiko hvy kwa mwanamke (mke) hasa ambae mmekaa kwenye ndoa zaidi ya miaka miwili na mkajaaliwa kupata watoto, yeye familia kwake ni yeye na watoto.
Na hili ni tatizo kubwa mno kwa wanawake wa vizazi vya Sasa. Mwanaume atafanya kila awezalo ili kuinusuru ndoa, lkn mwanamke mnaweza mkawa mnaongea ndani lkn tayari yeye keshakutoa ktk hesabu zake, yaani anakuwa hayupo kwa maslai ya kulinda ndoa, Bali yupo kwa maslai ya watoto.
Ndoa nyingi mno mjini zinapumulia mashine sababu ya uzembe wa wanandoa wenyewe lkn pia uzembe wa wanawake wenyewe kushindwa kuwa wavumilivu na consistent ktk ku absorb changamoto za ndoa lkn pia mapenzi kwa baba. Ushauri wangu kaa nae chini mzungumze na umueleze umuhimu wa yeye kuonesha mapenzi yake kwako Kama zamani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi unajua kuwa binadamu huwa tumetofautiana sana? Hasa ni kigezo gani ulichotumia kusema, ''sisi wanaume tupo hivi'' na ''hao wanawake wako vile'' Unapochambua jambo jaribu kuwa specific katika kile kilichopo mezani. Mada ni kuwa mapenzi yameamishwa kwa watoto. Kwajinsi mada ilivyoletwa si rahisi kuhukumu upande wowote kwani hatujui kinachoendelea in their day to day interactions.
Pili mnapoamua kuongeza familia kuwa na watoto, kuna baadhi ya vitu inabidi kuvi sacrifice au kuvi balance kwa miaka kadhaa hasa pale watoto wanapokuwa bado wadogo sana. Pia kumbuka kwa jinsi wanawake walivyoumbwa, wanakuwa na mapenzi yasiyo kifani kwa watoto hasa wanapokuwa bado wadogo, hii huja automatically tu.
Yote kwa yote couple inahitaji kuwa na mijadala ya kina jinsi ya kukabiliana na changamoto hizi na kuchukua initiative za kubalance romance na mapenzi kwa watoto.
mandela1
Inategemea wewe na mke mnaishi vipi na mjiwekea malengo gani ya ndoa yenu. Mimi kabla ya watoto tulikuwa very close mpaka nikawa naitwa briefcase ya mume wangu yaani hawezi niacha.
Baada ya watoto tukajiwekea malengo lazima tuwe na time hata masaa machache ya sisi wenyewe wawili tu. Basi tukajiwekea utaratibu either tunakula lunch au dinner pamoja nje ya home au tunakuwa na evening walk.
Mueleweshe kwamba watoto ni wapita njia, hawatakiwi kuchukua nafasi yako wala hawatakiwi kuwavurugia mipango yenu.
Asipoelewa, mchukue nenda nae kwenu au kwao, akawaone wazazi wake walivyobaki peke yao, bila shaka ataelewa watoto sio ndugu ni wapita njia tu!
Mkuu iko ivo, nadhani mzee wangu alianza kumzingua Bi mkubwa aisee Upendo wote maza ilibidi auelekezee kwangu na hivo ndo nilikuwa mtoto wake pekee wakiume.
Aisee! sijawahi pata upendo wa kweli kama ule umeni-affect sasa hivi nimekuwa na niko mbali na mama ila kwa siku lazima nimpigie Simu au anipigie zaidi ya mara moja asububi na jioni haiwezi kupita siku sijaongea nae kwa simu na naweza piga nae story hata nusu saa kwa simu.
Mkuu kuna mambo inabidi uelewe na ukubaliane nayo.
Swala la mwanamke kuhamishia mapenzi kwa mtoto hiyo ni nature na kamwe huwezi kuizuia wala kupambana nayo. Kumbuka mtoto anapozaliwa anakua helpless kwahiyo lazima kuwe na mtu wa kumuangalia, na ndio nature ikampa jukumu hilo mwanamke. Sisi wanaume hua hatuko attached saana na watoto zaidi zaidi ni kuleta matumizi tu.
Mistake kubwa tunayofanya waswahili ni kutokupangilia swala la lini tunapata watoto. Watu mkishaoana tu, mnafikiri kwamba ni lazima mpate mtoto as soon as possible! Wengine mnaoana na mimba tayari.
Wenzetu wazungu wanalielewa sana hili na ndio maana wao wanaweza kuoana na wakakubaliana kwamba mtoto wa kwanza tutapata baada ya miaka mitano. Hii inawapa nafasi kubwa ya kujivinjari bila bugudha na kufurahia mapenzi mpaka pale watakapoona sasa imetosha. Pia inawasaidia endapo wataachana hapo katikati kunakua hakuna watoto watakaodhurika kwani kisayansi ndoa nyingi huvunjika katika miaka michache ya mwanzo.
Kiuhalisia ni kwamba wakati wa kuenjoy mapenzi ni wakati mkiwa hamna watoto. Watoto wakishaingia, sahau habari ya mapenzi! By the time watoto wanawaacha nyie mmeshajizeekea wala hamna mzuka tena.