Mke wa mtu, Smart phone ya nini?

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
95% ya wake za watu wenye smart phone wanachepuka.Tangu lini mke wa mtu akawa na smart phone? Hizi ndo zinatumika kuleta usaliti mkubwa kwenye ndoa.Unakuta mke wa mtu yupo busy na mitandao, halafu mwanaume mzima na ndevu zako umetulia tu kama juha.

Mke wa mtu anatafuta nini mitandaoni kama siyo umalaya? Anachat nini na nani na kwa malengo yapi?Ni wakati wa wanaume kujitambua sasa, huo usawa wanaotaka wanawake haupo ng'oo!

Mwanamke anabaki kuwa mwanamke tu.Mungu alimtoa mwanamke katika ubavu tena wa kushoto wa mwanaume.Smart phone ni kwa ajili ya wanaume tu.

Mwanamke anaishi kwa mipaka mingi sana tofauti na mwanaume.Poleni wanaume wote ambao wake zenu wana smart phone, kuchapiwa hakukwepeki kabisa.
 
Mke wa mtu anatafuta JF umalaya?
au sijakuelewa?

Smartphone nayo ni umalaya?

na mke wa mtu kuendesha gari peke yake nayo itakuaje?
na kuvaa vizuri?
na kwenda shule?
Siamini kama jamaa ameandika alichodhamiria.
 
Kwa bandiko hilo lililojaa hasira zote,kuna moja kati ya haya mawili yamekukuta,
1.Umechapiwa mkeo/demu wako na ushahidi ukaupata kwenye smartfone yake au
2.Mtu wako wa karibu kachapiwa mke wake na ushahidi wa mazingira ukawaonesha kishawishi/kiunganishi cha mchapo huo ni smartfone anayomiliki huyo mwanamke.....
Yaan hakuna namna ni kukupa pole tu kiongozi na kukuambia siku nyingine yakikukuta ya kuchapiwa mkeo tena akiwa anamiliki nokia tochi, tafadhali usije kutangaza hapa maana kuchapiwa ni siri ya ndani.
 
Wew utakuwa umevurugwa si bure. . Sitaki kuamini kama hujui umuhimu wa social networks kwenye jamii. .mnunulie mkeo simu ya kitochi
 
Kweli ulichosema siuwongo pch wanazotuma huwa cizielewi inakuwa kama wanatafuta wateja yani kama biashara flani ivi imekuja kisasa zaidi mtandao kama badoo ni hatari kama mkeo yupo humo jitathimini mara 2
 
Saudi Arabia hawa viumbe hata gari hawaendeshi na kutembea hawatembei wenyewe kuna kidume lazima waongozane nae ,sometimes ubabe ni mzuri ila sijui kwa hili la smartphones
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…