Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,623
- 13,843
Kuna watu wanajiona ni wanaume na hata huwa wanaoa wanawake na kuzaa nao lakini kiuhakika wake si wanaume kweli.Kama wanawake wangekuwa si uwanawake wao basi wangewakataa mapema kabla ya ndoa.
Wanaume hao ninaokusudia wanajulikana kwa namna nyingi sana wa mwanzo kabisa ni wale wanaochukia wanawake na kuhimiza kutokuoa huku wakisimulia tabia za kike ambazo wao wanaziona ni kasoro bila kujua ndio maumbile yao.
Aina hiyo ya wanaume wakiombwa pesa na wake zao inakuwa ni nongwa kubwa na kuwaona ni adui zao badala ya kujua hiyo ni dalili ya mapenzi kwao kwani wameamua kufanya hivyo kwao japo wangeweza kufanya kwa wanaume wengine.Kama huna ficha aibu zako,toka katafute na bana matumizi.
Dalili nyengine ya wanaume hao ni wale ambao wake zao wanapokuwa na mimba au kuwa na wahka mwingine wa kimaumbile kwenye miili yao na wakawafokea,basi na wao hupandisha hasira na kufokeana nao mpaka ukazuka ugomvi na hata kupelekea talaka,
Mwanamume kweli huwa anabaki kimya hata maneno yakiwa makali namna gani au hutafuta njia ya kupenya na kuondoka akarudi baade kimya kimya bila kukumbusha wala kuuliza ilikuwaje.
Mwanamume wa aina hiyo akirushiwa kofi na mke wake basi anajibu kwa ngumi badala ya kuifutafuta na kumkimbia mkewe.
Mwanamume wa kweli ni lazima anakuwa na wivu na mke wake.Hawezi kumuacha kutoka peke yake bila kuwepo yeye mwenyewe au kumuambatisha na watoto.
Ambaye ni mwanamume wa kweli hakubali mke wake azungumze na wanaume wengine ambao si ndugu zake halisi na hawezi kumuacha mke wake akiwa maungo wazi yanayoonesha uzuri wake wote wachilia mbali kumuacha mke wake acheze disko na wanaume wengine.
Mwanamume wa kweli hamruhusu mke wake amuandalie chakula mwanamume mwenzie na kumsogezea mezani.Ikibidi hata kwenye banda la mama ntilie basi mwanamume wa kweli husogeza chakula mwenyewe kwa wateja
Msururu ni mrefu wa dalili za wanaume ambao si wanaume kweli baadhi yake zitaendelea hapo chini ,lakini nimalize na kusema wanaume ambao ni wanaume kweli hawawezi kuacha wake zao wapewe zawadi hata ya piipi na wanaume wenzao ambao si ndugu zao halisi.
Si kupokea tu bali hata kutoa zawadi kwa mwanamume yoyote yule asiyekuwa ndugu halisi wa huyo mwanamke.
Yote niliyoyataja hapo juu japo ni kwa uchache yakienda kinyume chake basi hupelekea talaka za mara kwa mara na za mapema sana.