Medecin
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 8,221
- 22,432
Mahakama ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imewapandisha kizimbani na kuwasomea shtaka watu watatu akiwemo Jovina Steven Mwekya (33), mkazi wa Mang'ula ambaye ndiye mke wa marehemu Mwalimu Tungaraza, Musa Amani Mwakyoma (28), mkazi wa Mang'ula, na Tadei Sales Mwinuka (40), mkazi wa Mang'ula, kwa kosa la mauaji.
Wakisomewa shtaka hilo na mwendesha mashtaka wa serikali, Dastan William, mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Regina Futakamba, amesema mnamo usiku wa Juni 2, 2024, wakati marehemu akiwa amelala chumbani, watuhumiwa hao walipanga njama ya kumvamia chumbani kwake na kumpiga na kitu kizito kichwani, hivyo kusababisha kifo chake.
Aidha, baada ya kusomewa shtaka hilo, watuhumiwa hao wamerudishwa mahabusu mpaka tarehe 25 Juni, 2024, itakapotajwa tena.
PIA SOMA:
- Morogoro: Atuhumiwa kula njama kumuua mumewe ili ale raha na bodaboda
Team kataa ndoa wanazidi kupata points za kugomea kuoa au kuolewa.