MKANGANYIKO KATI TFF NA ZFA NDANI YA MUUNGANO

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Wana jf leo asubuhi bungeni kumetokea mkanganyiko pale ambapo mbuge mmoja toka Zanzibar alipotaka kujua nini kitaikumba Tanzania katika medani ya soka kutokana na viongozi wa ZFA kupelekana mahakamani ili hali sheria za FIFA zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa mahakamani na adhabu yake ikionekana ni kufungiwa na FIFA. Kutokana na majibu ya waziri mwenye dhamana(Nape) yaligusia kuwa chombo kinachoiwakilisha Tz huko FIFA ni TFF, ndipo mbunge mwingine aliomba mwongozo na kusema kuwa waziri Nape ametoa majibu asiyokuwa na uhakika nayo kwani ZFA na TFF ni vyombo viwili tofauti akaenda mbali zaidi kuwa hata hiyo wizara ya Nape si ya muungano kwa kuwa mambo ya michezo na burudani si ya muungano. Je, ZFA wanatambulika FIFA? Kama hawatambuliki hilo swala likiwafikia FIFA nani atapewa adhabu ya kukiuka sheria za FIFA? Na km TFF hawana ubavu Zanzibar watajinusuru vp na huo mgogoro wa ZFA ili adhabu isijeikuta Tz kutokaFIFA? Na mbona kirefu cha TFF ni "Tanzania Football Federation", kwani Zanzibar haipo Tanzania?
Tujadilini kwa facts
 
Rasimu ya katiba ya warioba ilikuwa ni jibu na suluhisho tosha ila wasio na nia njema kwa hii nchi ndo wametufikisha hapa njia panda
 
Kwanini Kule Zanzibar nako kusiwe na mashirikisho ya mkoa tu na vyote vikawa chini ya TFF? Hivi wenzetu km vile vinchi vilivyopo UK vinafanya je? coz sijawahi ona Wales, Scotland ndani ya World Cup!
 
Kwanini Kule Zanzibar nako kusiwe na mashirikisho ya mkoa tu na vyote vikawa chini ya TFF? Hivi wenzetu km vile vinchi vilivyopo UK vinafanya je? coz sijawahi ona Wales, Scotland ndani ya World Cup!
Wacha ujinga!,wewe umeshawahi kuiona Tanzania ndani ya world cup? hizo nchi zimo World Cup na kama hujabahatika kuziona ndani ya world cup ndio sababu hizo hizo Tanzania hujaiona ndani ya world cup. Kimsingi hiyo ni moja ya hoja inayohaji uhalali kwa nini Zanzibar haiwezi kuwa mwanachama wa FIFA wakati nchi ulizozItaja ni wanachama wa FIFA?
 
Ccm mkoa wapi katika hili? Mje hapa na mtufafanulie na ubishi wenu
 
Siwezi kataa yawezekana nikawa mjinga kwa jambo fulani ambalo silijui, lkn si vizuri kumhukumu mtu kuwa mjinga kabla hujawa na uhakika km ni mjinga. Sikumaanisha kuwa hazionekani kwa sababu ya kutofudhu kufika fainali za kombe la dunia. Wales haina muda mrefu toka imeanza kushiriki ktk mashindano ya kimataifa..kuhusu Scotland sina uhakika unaweza kunipa fact.
By the way nisingependa sana tutumie kauli za kuonesha nani ni mwelevu ni nani mjinga coz I'm not a person of such a kind!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…