Msafiri Haule
Member
- Aug 6, 2018
- 28
- 18
Siku imepita lakini fikra hazikomi kunyukana baada ya kusoma gazeti la Mwanachi lenye kichwa cha habari “KUNI ZINAVYOKATISHA UHAI KWA KASI, JANUARY ASHTUKA”. Baadae, mikono nayo inanituma kutia wino yale yote kichwa hunena.
Yamkini watanzania wengi wamesikia/kuona ziara za Mh.Makamba (Waziri wa Nishati) katika kuhamasisha matumizi ya gesi, Kama njia mbadala kuepusha athari mbalimbali za kiafya hususani kwa “makabwela” watumia kuni.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Julai 12, 2022 (uk 3) nanukuu "Sasa natoa zawadi ya mitungi 300 kwa UWT ili iwe mtaji wa biashara kwa kinamama wa mkoa huu ikiwemo kuwakopesha ili kurahisisha shughuli za kupikia nishati safi".
Kutokana na andiko hilo, likashawishi kama Mtanzania ninayelindwa na katiba katika kutoa maoni, na ibara ya 18 (1)inasema “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati”.
Huku nikiamini kutovunja sheria na kufanya hivyo ni kwa kulinda mali za umma kama katiba inilindavyo hasa ibara ya 28 (2) inasema “Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao”.
Ikumbukwe kuwa, bajeti ya nishati kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni Shilingi 2,905,981,533,000 zakitanzania. Ambapo, Shilingi 2,823,029,576,000 sawa na asilimia 97.15 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,655,556,128,000 ni fedha za ndani na Shilingi 167,473,448,000 ni fedha za nje; na Shilingi 82,951,957,000 sawa na asilimia 2.85 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi 68,225,821,000 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) naShilingi 14,726,136,000 kwa ajili ya Mishahara (PE) yawatumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake, na hiyo ni kwa mujibu wa www.nishati.go.tz.
Hata hivyo, katika hotuba yako ya bajeti ya mwaka 2022/2023, unasema, nanukuu katika ukurasa wa 30, “Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Serikali itatekeleza mipango, mikakati na miradi ya matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia hasa maeneo ya Vijijini. Kwa ajili hiyo, tumetenga Shilingi Milioni 500 ili kufanya kampeni kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati bora ya kupikia pamoja na tafiti za kubaini nishati, mfumo sahihi na vivutio vya kusambaza nishati hiyo kwa maeneo ya vijijini”.
Kwa utangulizi huo, napenda kutumia ibara tajwa za katiba nahotuba ya bajeti kama kiongozi katika kuchagiza hoja na maswali yanayolindima kwangu na kwa wote wasio na “visemeo”.
Ndugu, Mheshimiwa Waziri,
Mosi, matumizi ya ziara hii yanaendeshwa kwa fedha za umma au ni bajeti tengefu ya CCM? Kama ni bajeti ya Serikali, kwanini ulijikita kwa wanachama wa CCM? Na nikifanya mapitio ya bajeti ya wizara ya nishati 2022/2023 iliyoidhinishwa na bunge na tayari imeanza kuwa sheria tangu tarehe 01/07/2022, nimelanda kona zote sijafanikiwa kuona fungu la zawadi katika matumizi ya wizara iliyochini yako. Je, unatumia sehemu ya bajeti hii ya 2022/2023 au ipi? Ni lile fungu la hamasa yaani milioni 500 za kodi za watanzania kutumika kama zawadi kwa jumuiya ya CCM?
Pili, Mh. Waziri, unataja matumizi ya kuni kama sababu ya vifo vingi, sina uthibitisho kulipinga hilo. Lakini, uzoefu unaniambia mabibi na mababu zetu waliishi miaka mingi zaidi. Katika maisha yao ni kuni ambazo ziliwawezesha kupika vyakula vyao nje kabisa ya matumizi ya gesi. Hebu tujadili kwa pamoja, tangu kugundulika kwa gesi mpaka hii leo wizara imejiridhisha pasi na shaka kupungua kwa vifo hutokana na watanzania kutumia gesi?
Ni watanzania wangapi leo hii hutumia hiyo nishati hususani vijijini? Tafiti inasemaje juu ya kumudu gharama za nishati hiyo endapo mtungi ukiisha, SISI MAKABWELA TUSIO NA MBELE WALA NYUMA, TUNAMUDU GHARAMA? Ikumbukwe kuwa, watanzania wengi huishi vijijini, na huko ndiko huzalisha chakula cha kutosha kukulisha hata wewe uliye mjini, na bado tunatumia kuni. Je, utafiti unaonesha kuwa gesi ni hitaji la msingi kwasasa ukilinganisha na vipaumbele vingine vyenye kugusa maisha yetu moja kwa moja kama vile mbolea?
Tatu, kwa kauli ya "sasa natoa zawadi..", kwanza itambulike kuwa kiambishi "na" katika "natoa" hudokeza nafsi ya kwanza umoja yaani "mimi". Je, tunaweza pokea uthibitishojuu ya ulichoahidi kukitoa ni chako wewe yaani kutoka mfukoni mwako pasi na kuhusisha mfuko wa kodi zetu?Kama siyo, kwanini utumie lugha ya umiliki ungali unajua wazi upo hapo kwaniaba ya serikali? Kwanini senti za umma zinatamkwa kama sehemu ya hisani binafsi? Hujui kama upo hapo kwa hisani ya jamhuri?
Nne, Zawadi hutolewa kama sehemu ya "motisha" kwa jambo fulani. Mfano, mzazi humzawadia mwanaye "baiskeli" baada ya kufanya vizuri darasani. Mh. Waziri, unatoa motisha kwa UWT ambao ni sehemu ya CCM ambapo wewe pia ni MwanaCCM, Swali, ni CCM pekee ndio wanaotumia sana kuni majumbani mwao? Je, mitungi hiyo wataiuza au kukodisha kwa watanzania wengine walio nje ya CCM? Unatuthibitishiaje hilo?
Tano, Taifa letu lipo chini ya mfumo wa vyama vingi kikatiba. Leo hii, ziara ya kiserikali tena siku ya kwanza tu, uelekeo ulikuwa katika jumuiya ya wanawake wa CCM na hapo hapo zawadi zikatolewa, Je, hakuna nia ovu ya ziara nzima ikiwamo kutumia fedha za umma kurejesha fadhila kwa Chama kilichounda serikali? Kwa yaliyofanyika, unaondoaje wivu kwa vyama vingine ili kututhibitishia nia njema ya ziara?
Sita, katika bajeti za wizara, mmeweka hadi fungu la zawadi?Licha ya malalamiko kuwa uchumi wetu umedolola sana, kwa sababu za UVIKO 19 na zile na vita ya UKRAINE, kumbe bado serikali inafedha nyingi hata kupata nyingine za kutolea zawadi na wakati huohuo bei za bidhaa zipo juu ikiwemo mafuta ambayo hapatikana katika wizara hiyo hiyo, Je, ni kweli taifa lipo katika kipindi kigumu au ni siasa hovyo kuruhusu mianya ya upigaji na uporaji wa mali za makabwela?
Saba, Sisi makabwela tunauliza, kutakuwa na uwazi kiasi gani katika mfululizo wa zawadi hizo walau tukaondoa shaka kupoteza senti zetu ambazo tunazitoa kwa shida kupitia kodi?
Nane, Watanzania tunawezaje kumtofautisha January Makamba ambaye ni waziri wa nishati na January Makamba ambaye ni kiongozi wa CCM. Je, makoti yote mawili unatamani uyavae wakati mmoja huku ukitumia mfuko wa umma katika agenda za kichama? Tunakutofautishaje?
Yangu ni hayo kwa leo, ingawaje sijakata kiu ya maswali ila, naamini nikijibiwa hayo machache, walau mimi na makabwela wenzangu tutapata nafuu ya mtafaruku katika minyukano ya fikra zetu.
Wasaalamu,
Msafiri Egno Haule
0758059818.