Mkakati wa Zambi na Mulugo kupinga mabadiliko ya Katiba ya CCM (mtu mmoja, cheo kimoja) wafichuka

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Kama nilivyoahidi tangu jana kuwa kuanzia leo tarehe 10 Machi 2017, nitaanza kuwaumbua wale wote wanaopanga na kushiriki mikakati ya kupinga mabadiliko ya Katiba ya CCM ambayo yanapangwa kupitishwa tarehe 12 Machi 2017. Hapa naomba nieleweke kuwa mtu kupinga mabadiliko ya Katiba si dhambi na wala si kosa la jinai. Chama chetu kilitoa muda wa kutosha kwa wajumbe kutoa maoni yao juu ya mabadiliko hayo. Hawa ninaowaumbua hawajafanya hivyo na badala yake wanatumia njia za kificho kueleza hisia zao.

Katika mtiririko wa kuumbua mikakati hii ovu, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa kutumia vyanzo vyangu ambavyo ni miongoni mwa wahusika wenyewe, nitaweka bayana kila mtandao unaohamasisha kupinga mabadiliko haya. Leo naanza na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbeya na Songwe.

Katika mikoa hii, vinara wanaoongoza kupinga mabadiliko ya Katiba ya CCM ni Mbunge wa Songwe, PHILIP MULUGO na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, GODFREY ZAMBI. Hawa wameunda Group lao la Whatsapp ijapokuwa Zambi hashiriki kwenye mijadala ili kuhofia ajira yake Serikalini na badala yake anawaelekeza viongozi wa CCM wilaya ya Mbozi nini cha kuchangia kwenye Group hilo baada ya kushauriana na Mulugo. wajumbe wengine kwenye Group hilo ni pamoja na;
  1. ALOYCE TUONEYE MDALAVUMA - Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbozi
  2. HEBRON KIBONA - Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Ileje
  3. DORIS JEREMIA KIMAMBO - Katibu wa CCM, wilaya ya Mbozi
  4. MALIKI NZOWA - Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Mbozi
  5. EDWARD MAHENGE - Mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka wilaya ya Mbozi
(Mniwie Radhi kama kuna jina nimelikosea)

KIPENGELE KINACHOPINGWA NA AKINA ZAMBI NA MULUGO NA SABABU ZAKE


ZAMBI na MULUGO wanapinga mabadiliko ya Katiba ya CCM hasa kipengele kinachosema MTU MMOJA CHEO KIMOJA. Viongozi hawa wanaona kuwa ikiwa Mabadiliko hayo yatapita, yatawabana yatawaweka njia panda juu ya wapi wagombee. Mathalan, kwa sasa, GODFREY ZAMBI ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mjumbe wa Halmashauri Kuu lakini wakati huo huo ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa ZAMBI anataka kugombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe wakati huo huo anataka kugombea Ubunge jimbo la Vwawa Uchaguzi Mkuu wa 2020. ZAMBI anaona kuwa ikiwa mabadiliko haya yatapita, yatamuweka kwenye wakati mgumu kuamua kama aendelee kuwa Mkuu wa Mkoa, au kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe au Ubunge Jimbo la Vwawa. Hataki kuipoteza nafasi ya Mkuu wa Mkoa ijapokuwa anatamani nafasi ya Mwenyekiti wa CCM na Ubunge. Vyote anavitaka.

PHILIP MULUGO kwa upande wake anavizia kugombea Uenyekiti wa CCM mkoa wa Songwe ikiwa Swahiba wake Zambi ataamua kuendelea na Ukuu wa Mkoa. Wakati huo huo anataka kugombea tena Ubunge Jimbo la Songwe uchaguzi mkuu wa 2020. Ni PHILIP MULUGO ndiye aliyeunda Group hilo la Whatsapp na Admin wake ni Katibu wa Ofisi ya Mbunge Jimbo analoongoza la Songwe.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbozi, MDALAVUMA anashinikiza Wajumbe wa Mkutano Mkuu hasa waliopo kwenye Group hilo wasafiri kwa Gari la CCM aina ya Toyota Landcruiser, Hard Top lenye namba za usajili T 554 BEW badala ya kutumia usafiri wa Basi kama walivyokubaliana hapo awali ili kupunguza gharama. MDALAVUMA anataka aende na gari hilo ili kurahisisha movement akiwa Dodoma hasa katika kuhakikisha mkakati wao unafanikiwa.

Nitoe wito kwa makada wa CCM nchi nzima. Zama zimebadilika. CCM mpya inazaliwa. Huwezi kuendelea kupinga mabadiliko then ukataraji kubaki salama. Lazima usombwe na mafuriko tu. Nimejitolea kuumbua maovu yanayotendeka ndani ya chama changu na nimefanya hivyo tangu 2014. Sipitwi na wala sishindwi kitu. Mnayopanga gizani basi mjue kesho yanawekwa hadharani. Nikusihi dada yangu Jesica Msavatavangu, ACHA.
 
Cheo kimoja, mtu mmoja. Hongereni kwa kufikiria vyema. Haya mabadiliko yataanza kuwa effected immediately? At last sasa Rais wa Nchi ataachia cheo cha Uenyekiti wa Chama
Hahahahahahaaaaa! Unataka Mwenyekiti wa CCM awe Lowasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…