Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) akabidhi ripoti ya 2014/2015 Ikulu

Madcheda

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
423
69
CAG wa Tanzania Prof. Juma Mussa Assad Leo saa 4 asubuhi amekabidhi ripoti yake ya mwaka 2014/15 kwa Rais Dkt. John Magufuli.

J11.jpg


IMG-20160328-WA0016.jpg
 
kwakuwa ni asad! Asad ajiandae kutumbuliwa kama hosea. Ila kunajipu moja JPM analilea nalo ni Beno Ndulu. Ndulu ni jipu
 
Nchi hii inavyeo vingi hadi vinasahaulika CAG, DCI,DPP, PCCB SIJUI PCM, UDA, SUMATRA, TBS, TFDA,NIDA,Yote vichaka vya kupiga mpunga wa mlala hoi. Mikoa mipya ndio usiseme Geita imekuwa mkoa huku haijawa hata Manispaaa, Chato imekuwa wilaya hata waijawa MJI mdogo, only in Tz
 
report ya ubadhilifu inafichwa kweli yaani...ishu ya mishahara hewa mbona report zingine kulikua hakuna wanakagua nini sasa kama vitu virahisi tuu havipo..
 
Waziri wa TAMISEMI alikuwa analilia hati chafu, alikuwa na hamu ya kuona halmashauri zinapigwa hati chafu.

Waziri hajui kabisa kutokana na inherent and control risks za halmashauri zetu CAG akiamua kukaza hakuna halmashauri hata moja inayoweza kupata hati safi.

Sio kwamba CAG alikuwa anazilea halmashauri hapana, mda mwingine serikali ilikuwa ikipewa grace period ya kutekeleza baadhi ya maagizo.

Sasa kitanuka mda si mrefu, huyu aliyekuwa analilia hati chafu atatia akili.

Leo kama sikosei mkuu Prof. Asad anawasilisha report na hati zake kwa Rais. Unajua halmashauri ngapi zimelamba hati chafu?

Ni kituko, tega sikio.
 
Kutoa hati chafu sio sifa bali wanatimiza wajibu wao wa kazi lakiniii hawa jamaa wanatuhumiwa kula mlungula sana ili watoe hati safi, ni muda muafaka wa kujitafakari
 
CAG timiza wajibu wako usizilee Halmashauri mbovu pia halmashauri zenye Hati chafu viongozi wake wangewajibika kuliko tunaishia kuwa wajirekebishe
 
Back
Top Bottom