Pre GE2025 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM- Mhandisi James Jumbe, ajinasibu kuwa CCM itashinda 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Aug 15, 2024
362
534
Yani kila mwaka CCM sera zao ni maendeleo sekta ya afya na elimu, miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado sera zao wanazoona zitawapitisha ni kama za miaka ya 70 huko.

Soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
===

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe, ameeleza imani yake kuwa CCM itashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 huku akitoa wito kwa wanachama na viongozi wa chama kuendelea kudumisha mshikamano ili kuhakikisha ushindi wa CCM.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo leo Februari 18, 2025 imetembelea kata ya Mwamalili na kata ya Old Shinyanga ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mhandisi Jumbe amesema kuwa Rais Samia ameonyesha uongozi thabiti na mafanikio makubwa katika sekta muhimu kama vile miundombinu, elimu, afya, na utoaji wa mikopo kwa makundi maalum.

Amesema Rais Samia amefanya juhudi kubwa katika sekta ya afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba, ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, na zahanati. Vilevile, ameboresha sekta ya elimu kwa kuongeza mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kuajiri walimu kwa wingi.

Mhandisi Jumbe amewahimiza wanachama wa CCM kushirikiana kwa nguvu, kujenga chama, na kumuunga mkono Rais Samia pamoja na viongozi wa chama ili kuhakikisha ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2025.

Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini pia ameeleza kuwa utendaji wa Rais Samia katika utekelezaji wa Ilani ya CCM umekuwa wa kiwango cha juu huku akitaja kuwa ndiyo sababu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM walimpendekeza kwa kauli moja kuwa mgombea pekee wa urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Pia amempongeza Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza, akisema kuwa ni mtu mwenye heshima, mchapakazi, na mstahimilivu.
 
Back
Top Bottom