Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 222
- 1,827
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga ametangaza kuachia wadhifa huo ndani ya miezi mitatu kuanzia juzi Septemba 28, 2023 baada ya kudumu kwenye wadhifa huo kwa miaka 15.
Kutokana na uamuzi huo, Bodi ya wakurugenzi wa MCT imemteua Ernest Sungura, kushika wadhifa huo na hivi sasa anafanya taratibu za ajira na mafunzo yatakayomuwezesha afanye kazi kwa ufanisi zaidi.
Sungura alikuwa Mkurugenzi wa magazeti ya Uhuru na pia Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) lakini aliondolewa katika taasisi hiyo na Bodi yake (TMF) muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
Ernest Sungura
Uamuzi wa Kajubi kung'oka kwenye wadhifa huo aliupata miaka 15 iliyopita (2008) aliutangaza juzi katika Mkutano Mkuu wa wanachama uliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfPHR).
Akizungumza na wanachama wa MCT waliohudhuria Mkutano Mkuu, Kajubi alisema anaondoka kwenye wadhifa huo huku akijivunia masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha taasisi za kihabari na kuendesha Tuzo za Umahiri wa uandishi wa habari (Ejat) kwa miaka 14 mfululizo.
"Leo hii MCT tuna jengo letu pale Tegeta jijini Dar es Salaam na tumeongeza jingine la ghorofa mbili linaliendelea kujengwa.
"Tunajivunia kusaidia kuanzishwa kwa Jukwaa la Wahariri Tanzania, kuimarishwa kwa Shirikisho la Umoja wa Vilabu vya Uandishi wa Habari Tanzania, kutoa mafunzo na vifaa kwa waandishi wa habari," alisema.