mom jordan
New Member
- Jun 8, 2024
- 1
- 1
Mumbe ndio ulikubali ulotoka marekani
Umeletwa kama msaada wa chakula nchini
Kuongezwa virutubisho kuleta protini mwilini
Mbona nchi nyingi zina njaa ikiwemo sudan kusini
Mjumbe ndio mbona unatupeleka chaka jamani.
Mjumbe ndio una nini lakini kila siku yambo jipya mjini
Nasikia unahamaaisha miaka saba kwa mwinyi
Na kulazimisha fomu moja tu CCM ndani chamani
Na hakuna wa kupinga hilo hadharani

Mjumbe ndio wasifia kila kituw waziwazi hadharani
Hata lililokithiri kwa ubaya usoelezeka hadharani
Mbona tunakutegemea utuwakilshe huku jimboni
Unaishia kutuwakilisha kwa sarakasi na bwebwe bungeni
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Mjumbe ndio hutaki maovu yako yawe hadharani
Utayaficha kisingizio unalinda usalama na amani
Atakayehoji chamtemakuni atakiona na koreo mdoni
Natamani kusema maovu sina mwanasheria wangu jamani

Mjumbe ndio akikuchukua huna amani popote nchini
Atafanya lolote kisingizio amri ya kiongozi serikalini
Hivi hakuna sheria na haki kwa wasemakweli mahakamani
Nasikia wanajengewa nyumba mitaani kisingizio mkubwa serikalini
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Mjumbe ndio nasikia unaitwa chawa wa mama
Kila baya ufanyalo kisingizio nimetumwa na mama
Kwani mama hajukutuma kuangalia usalama
Huku mtaani watoto wamama wanachofanywa ni unyama
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Mjumbe ndio nauliza tuna uhuru wa kujieleza na habari
Mbona msema kweli kakamatwa kisingizio kibali
Naogopa kesho kuitwa centro natafuta maneno mazuri
mama unaupiga mwingi mitano tena wewe ni mamaa.....
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Mjumbe ndio unatuchosha mpaka nyuso zimetuchakaa
Hukunmtaani kumevurugika mambo ni mchakamchaka
Sukari bei mara saba eti mafuriko yamesababisha
Inaagizwa mbali ufaransa mbona kuna sukari Malawi na Uganda

Mjumbe ndio umepata wazo la kujitetea kwa uzembe wako mjini
Miradi isiyotekelezwa kisingizio covid naintini
Kwani duniani kote ilitokea kwetu tu Tanzania nchini
Ukachukulia na mkopo wa kuitwa pesa za uviko naintini

Mjumbe ndio vipi ajira BOT mbona haziwekwi hadharani
Ajira ofisini mishahara minono watoto wa wakubwa serikalini
Nasikia ualimu ajira za watoto masikini zinatangazwa bungeni
Eti tulokosa ajira tujiajiri uje tujiajiri wote shambani

Mjumbe ndio kwani nchi haina dira yaaendeleo
Kila mtawala ana mipango mipya ya maendeleo
Nawe ni mshangiliaji kwa vigeregere na ndelemo
Kwani hii si nchi moja au kuna nyingine kwengineko
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Nasikia mjumbe ndio akiharibu kazi anabadilishwa wizara
Hakuna watu wapya wa kufanya kazi kwa wizara
Kiko wapi chombo cha kusimamia maadili kwa watawala
Au kwao kipaumbele posho na minono mishahara

Umetajwa kwa ripoti ya CAG huwajibishwi mshauri wa mkulu
Umeteuliwa kuongoza na kufanya maamuzi takukuru
Umenunua nyumba gari na Dubai umefanya kufuru
Na hakuna wa kukugusa ni onyo kutoka kwa mkulu
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Nini maana ya uzalendo au kuvaa tai na skafu ya bendera ya taifa
Wananchi wakihoji na kuandamana eti wanaleta vurugu kwa taifa
Tunaumia kwa uchungu tukiangalia hili taifa
Mnatufanya tumlilie nakumkumbuka Nyerere baba wa taifa
Mjumbe ndio unatupeleka chaka jamani.
Nasikia sahivi mjumbe ndio hawajibishwi wala kujihudhuru
Atakayesema maovu ya mjumbe ndio nso ajuhudhuru
Kama unabisha kamuulize.... au basi mdomo koma...
Eti DP world ina faida zipi ... mimi nae litanikuta jambo...

Wananchi tufanyeje kumkabilli mnyonyaji mjumbe ndio
Au tubadili katiba inayompa kiburi mjumbe ndio
Au tulie na sheria za kumuwajibisha mjumbe ndio
Au tuandamane kwa amani anapokosea mjumbe ndio

Eti kuna bunge mahakama na serikali ni mtatu mihimili
Wananchi tunasimama wapi kuikabili hii hali maana ni hatari
Naomba uchunguzi kwa watumishi na viongozi serikalini
Kwa utendaji mienenndo uwajibikaji na umiliki mali

Kwani mahakama inatoa tafsiri na sheria za nchi ipi
Jaji mkuu anateuliwa na kutenguliwa na mkulu serikalini
Atapataje ujasiri wa kumuwajibisha mkulu hadharani
Au miimili ipewe nguvu kikatiba kumkabili mjumbe ndio nchini

Wananchi vipi kuhusu chaguzi zijazo.... tunataka mabadiliko
Tulimpa dhamana mambo alofanya ndivyosivyo
Hatma ya maendeleo yetu ipo wapi... tunataka mabadiliko...
Kwani kula si tunapiga na matatizo kila uchwao

Au tufanye maandamano ya amani kutembea kote barabarani
Kuonyesha viongozi madarakani yaliyopo kwetu moyoni
Mengi magumu huku uswahilini na dhiki nyingi mtaani
Kula kwa jaaho jingi na maumivu mengi moyoni

Turekodi ahadi za watawala waombazo majimboni
Wasipotimiza tuwawajinishe na kuwatia hatiani
Kukomesha ahadi hewa kutoka kwa wawakilishi serikalini
Twateseka kwa dhiki wakifurahia posho nono bungeni

Mtuweke wazi hadharani mapato na matumizi serikalini
Kodi tozo zatuumiza mitaani hatuoni matokeo hadharani
Kuna mikakati ipi serikalini mbona safari haziishi ughaibuni
Maendeleo yanayotekelezwa ni misafara na safari za mbali

Eti kazi ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia serikali
Mbona nasikia bunge ni chama cha wajumbe ndio walahi
Eti nchi ina... songesha nipigetafu tigonivushe... nimbaya hali
Mbona mtaani hali tete pesa hakuna na ukavu mifukoni

Nini kifanyike nauliza nini kifanyike kuinusuru hii nchi
Eti hatma ya maendeleo na mageuzi ipo kwa wananchi
Au tumelala kitandani tuamke kwenye huu mnene usingizi
Alisema alisema alisema nyerere alisema vijana wote tuamkee....