Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,049
- 13,866
Mkoa wa Mjini Magharibi ni moja kati ya mikoa 31 ya Tanzania na unapatikana ndani ya Kisiwa cha Unguja. Mkoa huu una wilaya tatu ambazo ni Mjini, Unguja Magharibi A na Unguja Magharibi B.
Mkoa huu una wakazi takriban 893,169 kulingana na sensa ya mwaka 2022. Jimbo la Pangawe linaongoza kwa kuwa na watu wengi (93,763) likifuatiwa na Jimbo la Mwera ambalo lina idadi ya (watu 89,056). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Amani ambalo lina watu 20,626.
Soma pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mkoa wa Mjini Magharibi una jumla ya Majimbo 17, Baraza (Wilaya) 17 na Wadi 43.
Majimbo ya Mjini Magharibi ni pamoja na;
- Malindi
- Shaurimoyo
- Chumbuni
- Amani
- Magomeni
- Mpendae
- Jang'ombe
- Kwahani
- Bububu
- Mwera
- Welezo
- Mtoni
- Mwanakwerekwe
- Pangawe
- Fuoni
- Dimani
- Kiembe Samaki
2024
2025
Januari
Februari
- CCM yawahimiza vijana na madereva wa Boda boda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
- Tauhida Gallos Nyimbo ateta na Viongozi, asisitiza kujiandikisha kwenye saftari
- Zanzibar: Polisi wakanusha taarifa ya Mjumbe wa Kamati Kuu ACT kudaiwa kutekwa na vyombo vya ulinzi, wasema alikamatwa na kuachiwa kwa dhamana