Mji Ambao Kubeba Silaha Ni Wajibu

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
6,168
14,469
Screenshot_20241229_152003_Chrome.jpg


Kennesaw,Georgia ni mji mdogo wa kusini Marekani. Harufu ya mikate inayonukia kutoka kwenye tanuri mikate ya Honey suckle Biscuits &bakery,huku kwa mbali sauti ya treni ikisikika

Ni sheria iliyopitishwa mwaka 1980 inawalazimisha wakazi wa mji huo kumiliki kubeba silaha na bunduki,kwa kuhakikisha usalama na ustawi wa ujumla wa jamii na wakazi wake

Kila mtu wa familia anayeishi ndani ya mipaka ya mji huo anahitajika kumiliki bunduki pamoja na risasi zake "sheria na kanuni inasema wazi"

Sheria hii haiwalazimishi watu wenye ulemavu au wenye matatizo ya akili,na vile vile haiwahusu watu ambao wanakabiliwa na makosa ya jinai,na wale ambao sheria inapingana na imani zao za kidini

Na hakuna mtu ambaye ameiambia bbc ni adhabu gani inatolewa kwa mtu ambaye hatekelezi sheria hii. Kwa wakazi wengine wanaona fahari kwa kuwepo sheria hiii lkn kwa wengine wanaona aibu kuwepo kwa sheria hii.

Blake Weatherby mchekeshaji katika kanisa la baptist la kennesaw,, ana maoni yake kuhusu kwanini viwango vya uhalifu na vurugu vinaweza kuwa chini

Anasema " sio bunduki zinazo shusha uhalifu hapa kennesaw bali ni mtazamo" anaendelea kusema " iwe ni silaha,uma,ngumi au viatu virefu tunajilinda sisi wenyewe na majirani zetu

Makala moja ya mwaka 1982 katika gazeti la New York Times ilisema kwamba Viongozi wa Kennesaw wazi wazi walifurahia kupitisha sheria hii

Sheria za silaha kama hizi zimepitishwa katika miji mingine kama Gun Barrel City,Texas,Virginia na Utah. Mkulima wa bustani ya kanisa ambaye amezaliwa wakati ambao sheria za kumili bunduki zilianzishwa na kutekelezwa

Alifundishwa kwamba "kama wewe ni mwanaume unapaswa kumiliki bunduki" hivi sasa ana miaka 42,na alifyatua risasi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 12

Anaendelea kueleza kwamba wakati fulani alimiliki bunduki hadi 20,lakini kwa sasa hamiliki hata bunduki moja. Aliuza bunduki hizo ili ajikwamue kimaisha,ikiwemo na bunduki aliyoachiwa na baba yake alipofariki mwaka 2005.

Anasema " alihitaji gesi ya kupikia zaidi kuliko bunduki". Mkazi mkoja wa kennesaw anayejulikana kama Chris yeye hapendi sheria ya kumiliki bunduki na kusema " Najihisi vibaya watu wakizungumzia kuhusu sheria za bunduki"

Anataka wageni wa mji wake wavutiwe na mbuga za wanyama,shule na maadili ya jamii wanapofikiria mji wake na sheria za kumiliki bunduki

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom