Mjadala: Sheria gani inawapa mamlaka polisi kupiga na kuwanyanyasa watuhumiwa

James Hungury

JF-Expert Member
Jun 8, 2013
825
612
Habar wadau,

Nina swal nataka nijue,pengine tukijadil tunaweza pata majibu sahihi kwa pamoja.


Nimekuwa nikishuhudia na kuona baadhi ya askar wetu wa tz wanavyokuwa wakifanya mambo ambayo kwa ujumla yanatoa mashaka sana na utendaji wa jeshi letu.


Unakuta askar amemkamata mwalifu,badala yakumkamata na kumweka kwenye gar zao basi naendelea kumpiga na kumtukana au kumfanya vyoyote bike.


Zaidi mtuhumiwa anapofikishwa kituoni basi polisi huendelea na manyanyaso yasiyo ya maana kabisa na wakati mwingine hupiga watuhumiwa au kuwafanya wanavyohitaji wao.

Maswali ninayojiuliza

1. Mtuhumiwa ana haki gani anapokamatwa na polisi, je kuna sheria inayokuhusu askari kumwita mtuhumiwa jambazi, so mwizi au kumpiga, kumtukana kabla ya mahakama kutoa hukumu?

2. Je, ni sahihi polisi kumpiga, kumpiga, kumdhalilisha, kumnyima haki mtuhumiwa akiwa kituoni? Je sheria iko vipi?

3. Mwisho, kwanini askari wetu huwa wanatumia nguvu sana kwa hata watuhumiwa walio mikononi mwa sheria?

Naomba tujadili mada hii, kwa mifano hai tukiyokutana nayo, tupate elimu.

Thanks.

Nawasilisha
 
Shida yako umeandika na kujijibu humo humo yaan naona chapisho lako lina miziz ya kisiasa

ila kama the issue ilikua n sheria IPI ina mruhusu askari kutumia nguvu pale inapobidi iko sheria hii The police force and Auxiliary services Act kifungu cha 5(1)

Anaeza tumia pale inapobidi ,
 
Hakuna sheria inayowaruhusu kupiga kama mtu anatii amri, hata wanapokamata hawaruhusiwi kupiga.
 
Umekula vitasa huenda!!!! By the way Mtuhumiwa aliyekamatwa na askari kisheria haruhusiwi/ hatakiwi kupigwa, lakini endapo mtuhumiwa akionyesha ubishi sheria inamtaka askari police kutumia nguvu ya kiasi ( may use little force) !!
Note; NANI ANAWEZA THIBITISHA KUWA ULIPIGWA KWA UKAIDI? Hapo ndio panashida; kwahiyo ni rahisi kusema rituhumiwa ririkuwa rinareta kaujeuri! Hata kama hukuwa kaidi utaonekana kaidi tu.
 
Hapo kuna mambo mengi.

Kwanza,hakuna sheria ya kumnyanyasa na kumdhihaki wala kumpiga mtuhumiwa.

Pili,inategemea aina ya mtuhumiwa anayeenda kukamatwa ni wa aina gani,kama ni wa hatari lazima polisi wajihami na Kuchukua tahadhari kwa kutumia silaha,pingu na n.k

Tatu,kama mtuhumiwa anaonesha resistance ya kukamatwa ni lazima nguvu itumike kum arrest kwa tahadhari kubwa sana kwasababu hata Polisi anaweza kupata madhara.

Nne,mtuhumiwa hatakiwa kunyanyaswa kwa namna yoyote ile au kudhihakiwa na Polisi aidha kwa kutukanwa au kusemewa maneno mabaya.

Tano,Polisi wanapom arrest mtuhumiwa katika hali ya kawaida na usalama lazima wajitambulishe kwa na kutoa sababu za Kum arrest na sehemu wanakompeleka.
 
Niliumia sana siku Polisi na Mgambo wa Jiji la Mwanza walivyompiga kwa ukatili yule Machinga mwezi Januari. Yule Mmachinga aliyekuwa amechuchumaa bila ubishi huku ameshikilia nguo zake. Nashangaa watetezi wa haki za binadamu walijifanya hawakuona tukio lile lililoonyeshwa kupitia ITV.

Vv
 
Hawana mamlaka yoyote,wakitaka kukukamata piga garagaza wasikuzingue.
 
Sio little force bali ni reasonable force, issue hapa ni kuwa how reasonable is reasonable? mpaka leo mahakama haijaweza kudefine, kwa hiyo Polisi anaweza kukupiga kirungu kwenye viwiko ili kukuincapacitate na hatimaye akuweke chini ya ulinzi, otherwise utaratibu wa kumkamata mtu umeainishwa vizuri sana isipokuwa kwenye mazingira ya ambush ndipo changamoto inapoanza.
 
Polisi wana inferiority complexities hujawahi ona tena wengi nadhani wanaichukia kazi yao ya upolisi...
 
Ukijifanya mjuaji lazima ule kipondo tena kisawasawa pale unapokamatwa usibishebishe kubali muende kituoni

Vinginevyo mbona hizo ulotaja kidogo na wanapaswa hata wakudumbukize kwanza kwenye dimbwi la maji machafu halafu upake powder kidogo mpaka akufikishe kituoni ushakuwa kama mtoto wa kitimoto ili kesho usiwe jeuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…